Body

Swahili Devotionals

KUTENDA IMANI

David Wilkerson (1931-2011)

Imani ni amri na Mungu hujibu kwa wale wanaoitenda. Ushahidi mwingi ulioandikwa tunapokea katika ofisi yetu una ukweli huu. Katika kila tukio wakati mwamini alitenda ukweli wa Neno la Mungu, Yesu alikuja kwa mtu huyo. Na Roho yake ya utumishi iliwaletea faraja na kuimarisha nguvu zao wakati wa giza.

Bila shaka, si rahisi kila wakati kutenda imani tunapoumizwa. Mara nyingi hatuwezi kuwa na nguvu wakati maumivu yanatudhuru sana. Wakati huo Wakristo wanaweza kuacha ahadi za Mungu kuwa mbali nawo.

KUPITIA KILA JARIBIO

David Wilkerson (1931-2011)

Tunafanya uchaguzi ya kuishi maisha yetu yenye kujaa hofu kilamala au yenye kuamini mu Mungu. Ikiwa leo tunaruhusu sisi wenyewe kuwa na wasiwasi juu ya jambo moja, tutakuwa na wasiwasi kuhusu mambo mawili ya kesho. Kwa kifupi, hofu zetu zitaendelea kuongezeka kuwa mulima, kama mawimbi ya matatizo yataendelea kuja. Na kisha, ikiwa hofu zetu hazikaguliwe, akili yetu yakuwa nawasiwasi itaendelea kushuka kwenye shimo la chini.

KUOMBA KWA FURAHA

Gary Wilkerson

Mtume Paulo alikuwa mtu asiye na hofu. Je, alipataje kujiamini na furaha kama hiyo kati kati ya magumu, kutokuwa na uhakika, na upinzani? Ni aje tunawezaje kupata usawa kama huo katika wakati tunayoishi?

Kwanza kabisa, unapoumizwa maumivu ya wengine, Mungu atakuletea furaha! Watu wengi leo wanaumizwa kwa sababu ya kitu - kazi iliyopotea, kuchanganyikiwa au kushindwa kati ya mme au mke, ugonjwa wa kupungua, mpendwa anayepambana na umasikini.

KUWA MFUASI WA KRISTO

Nicky Cruz

Wakati macho yetu alifunguliwa na Yesu - tunapowaona watu jinsi anavyowaona - hatuwezi tena kukaa kimya wakati nafsi yenye kuumia kutembea bila niya kupitia maisha yenye kutuzunguuka. Huruma kwa waliopotea haiwezi kuishi pamoja na kutokua na shauku. Kukata taama hakutakua tena chaguo.

NANGA YA NAFSI YAKO

David Wilkerson (1931-2011)

Kwakuomba kwa imani, Mfalme Daudi alishika ukweli huu: "Mkondo usinagharikishe, wala wilindi visinimeze, wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu" (Zaburi 69:15). Sio kawaida hata mtu anaye kuwa karibu sana na Mungu anaweza kukabiliana na shida zinazoongezeka kama maji ya gharika. Na kama Daudi, tunaweza kudumbukia katika Neno la Mungu, kuwa mwaminifu kwa kuomba na kujitolea kwa Bwana, tena tunaweza kujisikia tunasumbuliwa na mawimbi ya hofu.

NENO LA MUNGU LINAZUNGUMZA KWA SAUTI KUBWA ZAIDI

David Wilkerson (1931-2011)

Huduma yetu ina tovuti ambayo hupokea ujumbe kutoka kwa Wakristo ulimwenguni pote. Hivi sasa waumini kutoka mataifa mbalimbali wanaandika kitu kimoja: Hofu inashikilia. Kama ilivyotabiriwa katika Maandiko, Mungu anatetemeza kila kitu kinachoweza kutetemeka na ni vigumu kutambua mshtuko wote unafanyika.

Katikati ya yote, wasiwasi unaenea na Wakristo hawana kinga. Wengi huandika kuhusu dhoruba kubwa katika maisha yao: migogoro ya kifedha, matatizo ya familia, kukosa huzuni. Wengine hushindwa zaidi na imani - na matatizo hayaonekani kuacha kuja.

MAANA YA UPENDO WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Wakati mume (au mwanamke) wa Mungu akiwa kwenye matengenezo, majeshi ya adui atakuja kwake kwa ghadhabu kubwa.

Je, unahonja kikombe kichungu cha maumivu, kudumu saa ya kutisha ya kutengwa na ya kuchanganyikiwa? Ikiwa ndio, nawahimiza kusimama kwa imani: "Kwamaana namujua yeye niliye mwamini, nakusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile" (2 Timotheo 1:12).

SEHEMU NGUMU ZAIDI ZA IMANI

David Wilkerson (1931-2011)

Yesu alisema huko Gethsemane, "Roho yangu ina huzuni nyi kiasi cha kufa" (Mathayo 26:38). Je, unaweza kufikiria Mwana wa Mungu akivumilia usiku wa kuchanganikiwa? Je, hakujua kwamba alikuwa karibu kudai ushindi wote juu ya kuzimu na kifo? Je, hakuwa na hisia ya ukoo ya muongozo na hatimaye, akijua kama Baba alikuwa pamoja naye?

Imesemwa na vizazi vya Wakristo kwamba sehemu ngumu zaidi ya imani ni nusu saa ya mwisho. Ninataka kuongeza neno hapa kwamba usiku mubaya wa kuchanganikiwa mara nyingi huja kabla ya ushindi, haki kabla ya giza kuvunja na mwanga hutokezea alfajili.

UKWELI, WA MAISHA MENGI

Gary Wilkerson

Wakati Roho inatufanya tuongeye kwa upendo, tunapaswa kufanya hivyo. Hivi karibuni wakati tulikua tunakula chakula cha mchana na mke wangu, nilihisi nia ya kumwambia mmoja wa watumishi wa mugahawa katika eneo letu kwamba Yesu alimpenda. Hakuwa na jibu lakini baadaye nikamwona akiwaambia wafanyakazi wengine kile nilichosema, ambacho hatukutalajia kukiona. Kisha jambo la kushangaza lilifanyika. Tulipokuwa tukiondoka, mhudumu tofauti alinisimamisha na kuwuliza kama ningependa kuomba pamoja naye!

RATIBA YA MUNGU

Carter Conlon

Wakati Mungu anasema, "Nitatumia maisha yako kwa ajili ya utukufu wangu," mara nyingi tunasahaulika kwamba upanga hautengenezewe kutoka kwenye mti, bali hutengenezwa kuta kwenye kiyayusho. Kutakuwa na joto, kunyoosha, kukunja, na kunoa tena kutazama tena. Yote ni muhimu, na itachukua muda. Hata hivyo katika mchakato huo, tunasema, "Bwana, nilifikiri kama unasema unaenda kutumia maisha yangu, lakini yote ninayofanya nimejikuta nikipitia kwenye moto. O, Yesu, nisaidie!”