MAANA YA UPENDO WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Wakati mume (au mwanamke) wa Mungu akiwa kwenye matengenezo, majeshi ya adui atakuja kwake kwa ghadhabu kubwa.

Je, unahonja kikombe kichungu cha maumivu, kudumu saa ya kutisha ya kutengwa na ya kuchanganyikiwa? Ikiwa ndio, nawahimiza kusimama kwa imani: "Kwamaana namujua yeye niliye mwamini, nakusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile" (2 Timotheo 1:12).

Roho yako inaweza kuwa haina mafuriko ya furaha na amani kwa wakati huu. Kwa kweli, bado unaweza kuwa na shida katika roho yako. Ikiwa ndivyo ilivyo, aca mizizi iwe imara katika Neno lake na acha kujaribu kufikiri kupitia njia yako kwahayo yote.

Naweza kukuhakikishia kuwa Mungu hakukusahau. Anaweka kwenye chupa kila chozi unadondoa. Asubuhi moja, baada ya kuhubiri mala ya kwanza neno hili, nilisogelewa na dada mpendwa ndani ya Kristo. Aliniambia, "Mchungaji, nilipokuja kanisani asubuhi hii nilikuwa na furaha na kuwa sina wasiwasi. Lakini wakati ulianza kuzungumza juu ya kikombe cha maumivu, nililia ndani. Nilitambua kwamba nimewekwa kwenye musitari wamebere. Mume wangu ameniacha na watoto wangu wanasumbuliwa. Nimeifunika ili nifiche maumivu yangu. Lakini kwa kweli, roho yangu inajaa mafuriko na huzuni." Niliomba pamoja naye wakati huo, nikimwomba Mungu afanye imani yake iwe kamili zaidi. Aliondoka na moyo wa kweli kwa sababu anajua yule amemwamini.

Ndugu mtakatifu, katikati ya vita vyako, umfanya Yesu kuwa furaha na matumaini ya maisha yako. "Huenda kilio huja kukaa usiki, lakini asubuhi huwa furaha" (Zaburi 30:5).

Mungu anafanya kazi yake bora ndani yetu wakati wa majaribio. Hebu acha atumie moyo wako ili hali yako isikusumbuwe tena. Kisha, chochote kinachoweza kuja, utakuwa juu ya hayo yote, ulieketi pamoja naye katika maeneo ya mbinguni. Wewe ni maana ya upendo wake wa ajabu!