NANGA YA NAFSI YAKO

David Wilkerson (1931-2011)

Kwakuomba kwa imani, Mfalme Daudi alishika ukweli huu: "Mkondo usinagharikishe, wala wilindi visinimeze, wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu" (Zaburi 69:15). Sio kawaida hata mtu anaye kuwa karibu sana na Mungu anaweza kukabiliana na shida zinazoongezeka kama maji ya gharika. Na kama Daudi, tunaweza kudumbukia katika Neno la Mungu, kuwa mwaminifu kwa kuomba na kujitolea kwa Bwana, tena tunaweza kujisikia tunasumbuliwa na mawimbi ya hofu.

Tazama utukufu wa Mungu wetu ni nanga ya nafsi zetu. Ina maana ya kujenga imani yetu katika saa hii ambapo wengi wanahisi kuwa wamejaa hofu. Ninaamini kanisa linahitaji jambo moja kwa wakati huu muhimu: ongezeko la ufunuo kuhusu ukubwa wa Mungu. Hivyo watu wengi wena wasiwasi duniani kote wanageukia kwa miungu kati kati ya hofu kali. Lakini wafuasi wa Yesu wanahitaji kukumbushwa nguvu na ukuu wa Mungu mmoja wa kweli.

Katika kitabu tulichapisha Ushindi Kupitia Tatizo, Wakristo wanachangiya ushuhuda wa msaada wa Mungu wakati wa majaribio yao magumu. Katika kila kesi walipata tumaini katika ufunuo wa ukuu wa Mungu.

Ushuhuda huu ulionyesha wazi kwamba wakati wa mafuriko ya taabu, watu wa Mungu wana chaguo. Chaguo letu la kwanza kwa kukabiliana na majaribio makubwa ni kuimarisha imani yetu - kuamini Baba yetu wa mbinguni mwenye upendo bila kujali nini kinachokuja.

Kila mtu aliyechangia hadithi Ushindi Kupitia Tatizo alishuhudia kwamba walikuwa na chaguo la kufanya. Na wakati walichagua imani, Mungu aliwapa urafiki mpya na Yesu. Hivyo hii ilitokea wakati jaribio lao la uchungu lilikuwa mbaya zaidi. Daudi alishuhudia juu ya saa yake mbaya zaidi, "Maskini huyu aliita, Bwana kasikia, akamwokoa na taabu zake zote" (Zaburi 34:6). Tunapaswa kushawishiwa imara kwa nguvu ya uwezo wake, nguvu na ukubwa kwa niaba yetu