RATIBA YA MUNGU

Carter Conlon

Wakati Mungu anasema, "Nitatumia maisha yako kwa ajili ya utukufu wangu," mara nyingi tunasahaulika kwamba upanga hautengenezewe kutoka kwenye mti, bali hutengenezwa kuta kwenye kiyayusho. Kutakuwa na joto, kunyoosha, kukunja, na kunoa tena kutazama tena. Yote ni muhimu, na itachukua muda. Hata hivyo katika mchakato huo, tunasema, "Bwana, nilifikiri kama unasema unaenda kutumia maisha yangu, lakini yote ninayofanya nimejikuta nikipitia kwenye moto. O, Yesu, nisaidie!”

Bwana anajibu kwako, "Nilikuambia kuwa nitaenda kutumia maisha yako kwa ajili ya utukufu wangu! Lakini siwezi kukutumia mpaka utakapokuwa tayari.”

Nabii Habakuki akasema, "Maana njozi bado nikwa wakati ulioamuriwa, inafanya haraka ilikuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia ingojee, kwa kuwa haina budi kuja” (Habakuki 2:3).

Mambo ambayo Mungu alisema kwako yatatokea. Ikiwa Mungu alisema anaenda kuleta familia yako nyumbani, basi ataleta familia yako nyumbani! Ikiwa Mungu alisema atatumia maisha yako, basi atatumia maisha yako - lakini kwa ratiba yake, si yako.

Paulo aliwahimiza Wafilipi: "Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo yakweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote yatafakarini hayo” (Wafilipi 4:8, KJV).

Wakati mwingine Mungu anaweza kuonekana kuwa kimya, hata ingawa tayari ametuma jibu. Hata hivyo, linakutana na kila aina ya upinzani kabla ya kutufikia. Kizuizi hiki kinaweza kuwa ndani yetu kwa sababu tumesikiliza sauti zingine zinazozuia sauti ya Mungu. Katika jamii ya leo, tuna uwezo wa kusikiya sauti nyingi, na ambazo zinaweza kutuongoza katika mawazo yetu kuelekea kwenye njia isiyo sahihi. Lazima tuwe makini sana kuhusu nani na kile tunachosikiliza.

Carter Conlon alijiunga na jopo la wachungaji wa wa Times Square Church mwaka wa 1994 kwa mwaliko wa mchungaji muanzilishi, David Wilkerson, na alichaguliwa kuwa Mchungaji Mkuu mwaka 2001.