KUWA MFUASI WA KRISTO

Nicky Cruz

Wakati macho yetu alifunguliwa na Yesu - tunapowaona watu jinsi anavyowaona - hatuwezi tena kukaa kimya wakati nafsi yenye kuumia kutembea bila niya kupitia maisha yenye kutuzunguuka. Huruma kwa waliopotea haiwezi kuishi pamoja na kutokua na shauku. Kukata taama hakutakua tena chaguo.

Mtume Yohana anatuambia hivi, "Hivi ndivyo tunavyojua watoto wa Mungu. Na watoto wa ibilisi nao ni: Mtu yeyote asiyetendaa haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake" (1 Yohana 3:10). Je, Neno la Mungu liko wazi zaidi kuliko hili? Kuna mtihani wa kawaida kwa kila kitu kwa nia yakuona kama sisi ni wafuasi wa kweli wa Yesu, kuona kama sisi ni watoto wake wakweli, na kutuunganisha kwenye kiwango cha huruma zetu kuhusu wengine.

Yohana anaendelea kuandika, "Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndai yake huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendon a kweli. Katika hili tutafahamu kwamba tu wa kweli, nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake, ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote" (1 Yohana 3:17-20).

Wakati Roho Mtakatifu ameingia ndani ya mioyo na maisha yetu, akitujaza upendo na huruma vya Yesu, tunawaona watu waziwazi. Macho yetu anaangaa kwa furaha ya Bwana, na hatuwezi tena kutembea kama watu hizi siku zetu waliotupwa nje - Umasikini, dawa zakulevya, Ulevi, kuwa mwanachama wa kikundi cha majambazi, mwenye dhambi-bila kumwona, bila kusikia maumivu yake. Tunajikuta wenyewe kumsaidia kurejesha utukufu wake mbele ya Mungu. Tunamkumbatia, tunaliya pamoja naye, na kumpeleka ndani ya mikono ya uponyaji ya Yesu. Hiyo ndio inamanisha kuwa mfuasi wa Kristo juu ya yote.

Nicky Cruz, mwinjilisti wa kimataifa aliyejulikana na mwandishi mkubwa, alimgeukia Yesu Kristo kutokana na maisha ya vurugu na uhalifu baada ya kukutana na David Wilkerson huko New York City mwaka 1958. Hadithi yenye kushangaza ya kuokoka kwake ulisemwa mara ya kwanza katika Musaraba na Kisu kinacho chomoka (Cross and Switchblade) na David Wilkerson na kisha baadaye katika kitabu chake chenye kuliuzwa vizuri, kiitwaco: Kimbiya, Mtuto, Kimbiya (Run, Baby, Run).