KUTENDA IMANI

David Wilkerson (1931-2011)

Imani ni amri na Mungu hujibu kwa wale wanaoitenda. Ushahidi mwingi ulioandikwa tunapokea katika ofisi yetu una ukweli huu. Katika kila tukio wakati mwamini alitenda ukweli wa Neno la Mungu, Yesu alikuja kwa mtu huyo. Na Roho yake ya utumishi iliwaletea faraja na kuimarisha nguvu zao wakati wa giza.

Bila shaka, si rahisi kila wakati kutenda imani tunapoumizwa. Mara nyingi hatuwezi kuwa na nguvu wakati maumivu yanatudhuru sana. Wakati huo Wakristo wanaweza kuacha ahadi za Mungu kuwa mbali nawo.

C.H. Spurgeon, mmoja wa wahubiri wakuu katika historia, alipata shida kali-wakati wa zama zake hali hii ilikuwa inajulikana kama "kuchukizwa." Ni dawa gani Spurgeon alitumia? Alitumiya Zaburi. Ahadi za Mungu za kudumu zilikuwa chanzo cha pekee cha faraja kwa Spurgeon wakati ulimwengu wake ulionekana kuwa unaanguka karibu yaye. Wakati mhubiri mkuu hakuwa na nguvu ya kuzisoma mwenyewe, alikuwa na mtu wakuzimusomea kwa sababu alijua zitamletea faraja na nguvu. "Basi imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Mungu" (Warumi 10:17).

"Kwamaana mtu amawendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamutafutao" (Waebrania 11:6). Neno hili lina maana hasa kwa waumini wako kati kati ya jaribio. Bwana anasema, "Nina malipo yenu kwa ajili jaribio lenu, nimeweka baraka ya nguvu kwa ajili yenu wakati huu, na nataka uwe na hilo Nenda unafuata hilo!"

Tunapaswa kujiingiza sisi wenyewe kwa Neno la Mungu - kukumbuka ahadi zake, kuamini uaminifu wake na kushikamana na yale ya kweli. Ndio njia pekee ya kukata sauti ya pepo ya mateso.

Zaidi tunavyoelewa na kuamini ukuu wa Mungu wetu, zaidi tutakuwa tayari kwa siku zijazo.