KUOMBA KWA FURAHA

Gary Wilkerson

Mtume Paulo alikuwa mtu asiye na hofu. Je, alipataje kujiamini na furaha kama hiyo kati kati ya magumu, kutokuwa na uhakika, na upinzani? Ni aje tunawezaje kupata usawa kama huo katika wakati tunayoishi?

Kwanza kabisa, unapoumizwa maumivu ya wengine, Mungu atakuletea furaha! Watu wengi leo wanaumizwa kwa sababu ya kitu - kazi iliyopotea, kuchanganyikiwa au kushindwa kati ya mme au mke, ugonjwa wa kupungua, mpendwa anayepambana na umasikini.

Tunasoma katika Wafilipi 1:1: "Paulo na Timotheo, watumishi wa Kristo Yesu." Paulo alikuwa akisema, "Mimi ni mtumwa, mwenye aliuzishwa kabisa. Kristo ndio mambo yangu yote." Na kisha anaendelea kushughulikia kikundi kikubwa: "Kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walio Filipi, pamoja na maasikofu na mashemasi."

Nimependa hii kwa sababu miaka kumi tu kabla, alikuwa ameanzisha kanisa huko Filipi na mfungwa tu, mwanamke na msichana mtumwa. Sasa kanisa lilikuwa na wazee na mashemasi na maasikofu. Ilikuwa mupangiliyo na utaratibu wenye nguvu!

Kisha anasema katika mstari wa 2, "Neema na iwekwenu na amani zitokazo kwa Mungu." Hapa anaweka sauti katikati ya majaribu yetu kutufanya tutegemee neema, na amani inayotoka kwa chanzo kimoja tu, Mungu, Baba, na Bwana Yesu Kristo.

"Namshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo, sikuzote kila niwaombeapo ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha" (1:3-4).

Ninapenda jambo anasema, "Nawakumbuka ninyi nyote." Wakati mwingine tunakumbuka baadhi tu, sawa? Wakati mwingine hatupendi kuombea maadui zetu, wale ambao walituumiza au kutusumbua - watu vagumu kanisa au katika familia yetu. Lakini Paulo anasema, "Ninawaombea ninyi nyote na wakati wowote ninapoomba, ninaomba kwa furaha."