Body

Swahili Devotionals

TULIITWA ILI TUTUMIKE

David Wilkerson (1931-2011)

"Walakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu" (Wafilipi 2:19).

Hapa Paulo alikuwa ameketi katika kiini cha jela huko Roma, bila kufikiri juu ya faraja yake mwenyewe au hali yake ngumu. Alikuwa na wasiwasi tu juu ya hali ya kiroho na kimwili ya watu wake na akawaambia, "Faraja yangu itakuja wakati tu najua kwamba muko munafanya vizuri - kiroho na kimwili. Kwa hivyo ninawatumia Timotheo ili awahakikishiye nyinyi kwa niaba yangu."

ROHO MTAKATIFU, MWARIMU WETU

David Wilkerson (1931-2011)

Ikiwa moyo wako unahamasishwa na idhini ya wengine na hii inaathiri njia unayoishi, uaminifu wako umegawanyika. Utakuwa daima unajitahidi kumpendeza mtu mwingine kuzidi Yesu.

Miaka michache baada ya mtume Paulo kugeuka, alienda katika kanisa la huko Yerusalemu ili kujaribu kujiunga na wanafunzi huko. "Nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi" (Matendo 9:26).

USIWE NA WASIWASI KATIKA SALA

David Wilkerson (1931-2011)

Kuna matokeo mabaya kwa kukataa kuomba. Neno linasema, "Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii" (Waebrania 2:3).

Najua kitu cha kufanana kama kisima chenye maji aliokauka kutoka kwenye chemchemi, na kuikausha kila baraka katika maisha yangu. Hii ilitokea wakati wa siku zangu za kutojali kuhusu sala. Katika kipindi hicho, nilikuwa na wakati wa utulivu lakini hakuna ufanisi katika sala. Niliacha wasiwasi za maisha kuniiba muda wangu pamoja na Bwana.

FURAHA YA BWANA

David Wilkerson (1931-2011)

Wanafunzi walipomwambia Yesu, "Bwana, tufundishe sisi kusali" (Luka 11:1), ni kwa sababu walitaka kujifunza kusali kwa namna iliyompendeza. Hivyo hivyo, Wakristo wengi leo wangependa kuwa waaminifu katika sala - lakini hawajui jinsi gani. Kwa sababu hawajui kusudi la msingi la sala, hawana maisha ya maana ya sala.

WITO WA KUTOA

Gary Wilkerson

Katika miaka mitatu ya huduma, Yesu alikuwa anawaponya wagonjwa; alirejesha kuona kwa vipofu; alifufua wafu; miujiza mingi; aliwahubiri maskini habari njema; na kufundisha raia ukweli juu ya Baba yao wa mbinguni. Orodha ya kushangaza ya mafanikio yalitokea kwa sababu ya utii wa Mwana kwa mapenzi ya Baba.

KUWAWEZESHA WATU WA MUNGU

Jim Cymbala

Mwanzoni mwa huduma wazi ya Yesu, jambo la ajabu lilifanyika ndani ya sinagogi katika mji wa Nazareti. Akifanya kama msomaji mteule wa kifungu cha Agano la Kale kwa siku hiyo ya Sabato, Bwana alisoma maneno haya:

"Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa" (Luka 4:18-19).

DHAMBI YA KUTOAMINI

David Wilkerson (1931-2011)

Kutoamini kunahuzunisha moyo wa Mungu kuliko dhambi nyingine yoyote. Sisi Wakristo tunalia dhidi ya dhambi za mwili, lakini Mungu anahusika na dhambi za moyo - kuwa na mashaka juu ya Neno lake au kuwa na maswali juu ya uaminifu wake. Masuala halisi ya maisha na kifo ni mengi zaidi na jinsi mtu anavyofikiri kuliko kile anachofanya.

USALAMA KATIKA KILA HALI

David Wilkerson (1931-2011)

"Usiogope hofu ya ghafula, wala uharibifu wa waovu utakapofika. Kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako, naye atakulinda mguu wako usinaswe" (Mithali 3:25-26).

Watu wengi leo wanauliza maswali ambayo hawana jibu la uhakika. Je, kutakuwa na wasiwasi hivi karibuni? Je, tunakabiliwa na dhoruba kubwa ya kiuchumi ambayo mawaziri wengi na watalamu wa uchumi wameonya?

ILI NIWEZE KUJUA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu alimpa Musa maagizo ya kutisha: "Haya, ondokeni, katokeni hapo wewe na hao watu uliowaleta wakwee  kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, niliposema, 'Nitakipa kizazi chako nchi hii.' Nami nitamtuma Malaika wangu aende mbele yako . . . kwa maana mimi sitakwenda kati yenu; kwasababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu; nisiwaangamize ninyi katika njia" (Kutoka 33:1-3).

KRISTO ANAKUJA!

David Wilkerson (1931-2011)

Nabii Danieli alitabiri kampuni ya watu wa siku za mwisho iliyo na hekima na ufahamu katika mambo ya Mungu - waliosalia waliojitakasa, waliopimwa ambao wataelewa Neno lake. "Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa" (Danieli 12:10).