KUWAWEZESHA WATU WA MUNGU

Jim Cymbala

Mwanzoni mwa huduma wazi ya Yesu, jambo la ajabu lilifanyika ndani ya sinagogi katika mji wa Nazareti. Akifanya kama msomaji mteule wa kifungu cha Agano la Kale kwa siku hiyo ya Sabato, Bwana alisoma maneno haya:

"Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa" (Luka 4:18-19).

Yesu kisha akafuata usomaji wake wa umma kwa maneno haya ya ajabu: "Leo Maandiko haya yametimia masikioni mwenu" (Luka 4:21). Kifungu hiki maarufu kutoka Isaya 61 kilichosemwa juu ya Masihi ambaye Israeli alikuwa anamngojea. Yesu alijitangaza mwenyewe kuwa huyo aliyeahidiwa. Kwa hili aliwaelezea watu wa miji wake kwamba alikuwa zaidi kuliko tu walidhani kwamba alikuwa ni mwana wa seremala.

Juwa kwa makini kwa nini Yesu alitiwa mafuta na Mungu na kwa nini Roho alituwa juu yake akiwa na nguvu. Kusudi lake lilikuwa kuleta habari njema kwa maskini wenye tumaini la kidunia, kutangaza uhuru wa kiroho kwa wale waliofungwa na dhambi na Shetani, kutoa ujumbe wa wokovu ambao Mungu alitaka kila mtu asikiye na awe na uzoefu. Ndiyo maana Roho Mtakatifu amemtia nguvu Kristo kwa kushangaza - kusaidia watu wenye dhambi, watu wenye kuwa na mahitaji ili wapate njia yao ya kurudi kwa Mungu. Yeye hakupewa hivyo sisi Wakristo tuweze kuwa na mikutano ya kusisimua na wakati wa furaha ya kiroho, kama ajabu yakuweza kuwa hivyo.

Roho Mtakatifu alitumwa kukamilisha madhumuni mengi ya Mungu, lakini juu ya hayo yote ilikuwa kuwezesha watu wa Mungu kufikia ulimwengu na injili ya Kristo. Ikiwa tunapoteza maono ya moyo wa Mungu wa upendo kwa ulimwengu - ikiwemwo miji yetu na vitongoji – tutakuwa nauzoefu kidogo kwa nguvu za Roho, wakati sisi tuko kwenye ukurasa tofauti nawule wenye kuendelea wa Bwana wetu.

Jim Cymbala alianza na Brooklyn Tabernacle akiwa na wanachama wasio zidi ishirini katika jengo la chini katika sehemu ngumu ya mji huo. Mzaliwa wa Brooklyn, yeye ni rafiki wa muda mrefu wa David na Gary Wilkerson.