KRISTO ANAKUJA!

David Wilkerson (1931-2011)

Nabii Danieli alitabiri kampuni ya watu wa siku za mwisho iliyo na hekima na ufahamu katika mambo ya Mungu - waliosalia waliojitakasa, waliopimwa ambao wataelewa Neno lake. "Wengi watajitakasa, na kujifanya weupe, na kusafika; bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa" (Danieli 12:10).

Isaya alifadhaishwa na upofu wa kiroho kwa kurudi nyuma kwa Israeli na akasema, "Hukosa katika maono, hujikwaa katika hukumu" (Isaya 28:7). Uelevu mdogo ambao waliokuwa nao walikuwa wameharibiwa na tamaa zao, lakini Isaya aliendelea kuhubiri juu ya siku ambayo "viziwi wataisikia maneno . . . macho ya vipofu yataona katika upofu nakatika giza. . . . Wao wataritakasa jina langu; naam, watamtakasa Mtakatifu wa Yakobo [Kristo], nao watamcha Mungu wa Israeli. Hao nao wakosao rohoni mwao watapata kufahamu, na hao wanung’unikao watajifunza elimu" (Isaya 29:18, 23-24).

Ninaamini uamsho wa siku za mwisho ambao wengi wanahubiri, ni uamsho wa utakaso. Ikiwa kazi ya Roho Mtakatifu ni kuhukumu ulimwengu wa dhambi, haki na hukumu, basi ni hakika kwamba kumwagika juu ya wanadamu kutahusisha mawimbi yenye nguvu ya imani. Kanisa lenye kutojali, lenye kulegeza litatikiswa na kulazimishwa kukabiliana na dhambi zake.

Wakati makundi ya Wakristo yanatafuta ishara na miujiza, wakitafuta walimu wa mafanikio na utajili, Mungu amekuwa akiita nje "watu wa jangwani" ambao wanatumiwa na njaa ya zaidi ya Kristo. Wamechanganyikiwa kuhusu unafiki, watakatifu hawa wanaingia katika Neno la Mungu na kugundua madhumuni Yake ya mwisho. Wanajiweka wenyewe ili kusikia na kuelewa na Roho Mtakatifu kwamba mwisho wa vitu vyote uko karibu.

Kristo anakuja! Weka kando kila dhambi inaokusumbua na weka upendo wako kuhusu mambo ya juu! Msiwe washiriki katika ndoto za wanadamu, lakini jitayarishe kukutana na Mwokozi wenu.