ILI NIWEZE KUJUA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu alimpa Musa maagizo ya kutisha: "Haya, ondokeni, katokeni hapo wewe na hao watu uliowaleta wakwee  kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, niliposema, 'Nitakipa kizazi chako nchi hii.' Nami nitamtuma Malaika wangu aende mbele yako . . . kwa maana mimi sitakwenda kati yenu; kwasababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu; nisiwaangamize ninyi katika njia" (Kutoka 33:1-3).

Watu wa Mungu walikuwa wamepoteza kabisa mwelekeo kwa sababu ya tamaa na kuabudu sanamu (tazama Kutoka 32:25). Dhahabu ilikuwa ni mungu wao na yote waliyotaka kufanya ilikuwa kucheza na kufuata kutamani kwao. Wana wa Lawi tu ndio waliinuka kwa utakatifu wa Mungu.

Bwana alijiondoa kutoka kwao "asije kuwaua" lakini bado akawaambia, "Nitawapa yale niliyoahidi." Kwa hivyo wanaweza kudai haki zao zote na ulinzi wake - lakini sio uwepo wake.

Tunaona kitu kimoja leo. Matukio ya uingi wa watu wa Mungu wakiendelea katika jitihada zao za haki zilizoahidiwa wakati hawana utakatifu, kwakuhukumu uwepo wa Kristo.

Nadhani hakuna kitu kinachoweza kuwa kibaya zaidi kuliko kusikia hili kutoka kwa Bwana: "Nenda kwenye nchi imiminikayo maziwa na asali, lakini mimi sitakwenda pamoja nanyi" (angalia Kutoka 33:3).

Musa alitaka kitu kikubwa kuliko nchi inayomiminika maziwa na asali. Alitaka kujua na kuona uwepo wa Bwana! "Nipate kukujua, ili nipate neema mbele zako" (Kutoka 33:13). Haishangazi kwamba mtumishi wa Mungu mwenye thamani kubwa alihukumu kizazi chake! Haishangazi kwamba kulikuwa na utukufu mwingi kwenye uso wake. Alitaka kujua tu Bwana, kuishi karibu ya uso wake.

Leo nawahimiza kufuata mfano wa Musa. Na tuweze kusema pamoja na Paulo, ambaye moyo wake ulililia, "Ili nimjue yeye" (Wafilipi 3:10).