USALAMA KATIKA KILA HALI

David Wilkerson (1931-2011)

"Usiogope hofu ya ghafula, wala uharibifu wa waovu utakapofika. Kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako, naye atakulinda mguu wako usinaswe" (Mithali 3:25-26).

Watu wengi leo wanauliza maswali ambayo hawana jibu la uhakika. Je, kutakuwa na wasiwasi hivi karibuni? Je, tunakabiliwa na dhoruba kubwa ya kiuchumi ambayo mawaziri wengi na watalamu wa uchumi wameonya?

Hakuna mtu hapa duniani anayejua majibu ya kweli. Watalamu wa uchumi wanatoa utabiri wenye kupingana sana, na wanaoitwa manabii hutoa kila aina ya maonyo ya kuchanganya na yenye kusikitisha. Ninaamini kwamba unabii wote wa kweli lazima utowe tumaini na faraja kwa watu wa Mungu wanaoishi kwa imani.

Miaka michache iliyopita, mamia ya Wakristo wenye wasiwasi waliniandika kuhusu unabii ambao ulisema kwamba Florida ingekuwa imefulikwa na mawimbi. Wengi walitoka nje ya Florida kwasababu ya kilichojulikana kama likizo juu ya tarehe iliyotabiriwa - tu ikiwa hali ya unabii ilikuwa sahihi. Florida bado iko nasi.

Hakuna mtu anayejua wapi, jinsi gani, au wakati ambapo Mungu atatuma hukumu. Nyakati na misimu yote viko mikononi mwake. Je, Unakaa katika eneo la tetemeko la ardhi, labda karibu na mstari wa kosa? Au katika kitongoji kinachopanuka ambacho kinaonekana kuwa kina usalama mudogo siku zikiendelea? Hakuna chakula kilichohifadhiwa? Hakuna duka za dhahabu au sarafu za kukabiliana na mfumuko wa bei? Hakuna kurudi tena ikiwa uchumi umeanguka? Hakuna kitu cha uzima kinachoweza kuishi ikiwa unapoteza kazi yako?

Usiogope! Una kile unachohitaji ukiwa unaamini ya ahadi ya ulinzi wa Bwana. Zaidi nikusoma maneno ya Yesu, zaidi naamini anaomba uaminifu wetu kama wa mtoto - kutuweka salama katika kila hali.