TULIITWA ILI TUTUMIKE

David Wilkerson (1931-2011)

"Walakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu" (Wafilipi 2:19).

Hapa Paulo alikuwa ameketi katika kiini cha jela huko Roma, bila kufikiri juu ya faraja yake mwenyewe au hali yake ngumu. Alikuwa na wasiwasi tu juu ya hali ya kiroho na kimwili ya watu wake na akawaambia, "Faraja yangu itakuja wakati tu najua kwamba muko munafanya vizuri - kiroho na kimwili. Kwa hivyo ninawatumia Timotheo ili awahakikishiye nyinyi kwa niaba yangu."

Kisha Paulo alifanya kauli yenye kutisha: "Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakaeiangalia hali yenu kweli kweli" (2:20). Inasikitisha! Kama Paulo alivyoandika hili, kanisa la Roma lilikua na kubarikiwa. Kwa wazi, kulikuwa na viongozi wa kimungu katika kanisa la Kirumi lakini Paulo alisema hakuwa na mtu ambaye alishirikiana naye kimawazo ya Kristo. Kwa nini ilikuwa hivyo?

"Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu" (2:21). Kwa dhahiri, hakuna kiongozi mmoja alikua huko Roma aliyekuwa na moyo wa wutumishi; sio mmoja aliyepoteza sifa na kuwa dhabihu iliyo hai. Badala yake, kila mtu alikuwa ameanza kutekeleza maslahi yake mwenyewe. Hakuna aliyekuwa na mawazo kama ya Kristo na Paulo yakutomuwezesha kumtegemea mtu yeyote kwenda Filipi kuwa mtumishi wa kweli kwa muili huyo wa waumini.

Tunapoangalia mambo anazunguuka Kanisa la leo, tunaona mambo kama yale yale anayoendelea katika makanisa mengi. Wahudumu na wafuasi, sawa, wanafuata mambo ya dunia hii: pesa, sifa, mali, mafanikio.

Maneno ya Paulo hapa hayawezi kufadhiliwa: Kila mtu anajitokeza. Wahudumu hujitahidi kujifaidi wenyewe, kwa hiyo ndio sababu hakuna mtu ambaye ninaweza kumtumaini kutunza mahitaji yenu na kuumizwa - isipokuwa Timotheo.

Marafiki, tunaitwa kutumikia Kanisa la Yesu Kristo kama Timotheo, tunapaswa kuwa na mawazo ya dhabihu, upendo na wasiwasi kwa wengine.