A Heart After God

KATIKATI YA UTAMADUNI MBOVU

Gary Wilkerson

Kanisa la kwanza lilijikuta katika mazingira yanayofanana sana na ambayo tunajikuta leo. Walikuwa wakiishi chini ya utawala wa mabavu wa Roma na tamaduni yake isiyo ya kimungu, ya kipagani. Vurugu zilitukuzwa hadharani. Walikuwa wanakabiliwa na uasherati ambao ulizidi hata uharibifu mbaya ambao tunaona katika utamaduni wetu leo.