SIMAMA UPIGANE VITA

David Wilkerson (1931-2011)

Ni Wakristo wangapi wanaojiita mashujaa lakini hawajawahi kujaribiwa au kufundishwa? Tunasikia juu ya mashujaa wengi wa maombi katika taifa hili. Lakini ukweli wa kusikitisha ni kwamba, wengi wao hawajawahi kufunzwa - hawako tayari kupigana. Waumini wengi wa kweli wanakataa kupigana na ibilisi au kufanya vita dhidi ya ufalme wake.

Wakati Mungu anampata mwamini akiwa na njaa na hamu ya baraka yake, humtia ndani ya mu viriringo ili ajifunze kupigana. Bwana atahitaji mashujaa waliofunzwa vizuri ambao watashinda nguvu zote za kuzimu katika saa yake ya mwisho ya vita.

Hivi sasa Mungu anafanya kazi ya haraka katika mabaki yake - inaitwa mafunzo ya shida. Watakatifu hawa walijaribiwa katika mafunzo haya wanakuwa wakuu wa jeshi lake la siku za mwisho. Mungu anaweka vita vya Roho Mtakatifu ndani yao na anawaleta mashujaa waliopimwa na walijaribu, kwa sababu wamejaribu Mungu, kama vile Yakobo alivyofanya (ona Mwanzo 32:24-32).

Aina hii ya mafunzo inahitaji nidhamu ya mwili na kiroho. Yakobo alitupa mwili wake wote vitani, uwezo wake wote wa kibinadamu. Roho ya mapigano ilikuwa imeibuka ndani yake na maandiko yasema, "Alipambana na Malaika na akashinda" (Hosea 12:4). Aya hii ina maana kubwa kwa wale wote wanaotaka kushinda katika sala. Inasema Yakobo alikuwa mbere na akashinda vita. Ikiwa utashinda katika siku hizi za mwisho, itabidi kuweka nguvu zako zote ndani yake.

“Kuwa mwenye akili, na kukesha; Kwa sababu mshitaki wenu ibilisi, hutembea kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammezae. Nanyi mpingeni huyo” (1 Petro 5:8-9).

Wakristo wengi wanatarajia Mungu kwa njia fulani aokowe familia zao, kupatanisha uhusiano, kufanya miujiza, bila malipo kwao. Wanataka kupumzikia katika kiti chao kinachozunguka zunguka na "kumwamini Mungu kwa yote." Lakini suala hili la kujiweka katika maombi - "kuvunja kwa kupitia" kwa Mungu, kwa kupata majibu na kuona matokeo - itagharimu mwili wako kitu.

Mungu anataka umshike kwa sababu anakupenda. Yeye anataka umpe baraka zake zote. Inuka juu kwa imani na ushike ahadi Zake. Simama upigane. Una nguvu zake ili uzitumie!