MABALOZI KWA AJILI YA KRISTO

Gary Wilkerson

"Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu” (2 Wakorintho 5:20).

Kuwa "balozi kwa ajili ya Kristo" sio kitu tunachojitahidi kufikia. Ikiwa wewe ni Mkristo, wewe ni mmisionari. Hii sio maana tu kupelekwa nje ya nchi au kwenda kwenye ufikiaji. Ujumbe huu tulio nao unajumuisha kuwa na moyo unaompenda kwa namna ambayo tunataka kuona wengine wanajua upendo huo pia.

Napenda kuchukua mtazamo tofauti juu ya hilo na kukuambia sio tu kuhusu kutumwa; si tu kuhusu kufikia majirani yako. Ni kuhusu aina urivyo kama mmisionari

"Ole wenu waandishi na Mafarisayo,wanafiki!Kwa kuwa mu mnazuguka katika bahari na nchi ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili na Zaidi kuliko ninyi wenyewe” (Mathayo 23:15).

Hapa Yesu anasema, "Mnakwenda kutoka sehemu moja hadi nyingine mukijaribu kubadili mtu mmoja, mwongofu mmoja, na wakati unapopata hiyo, wao ni wabaya zaidi kuliko ninyi." Kwa wazi hiyo sio uinjilisti mzuri!

Hivyo ujumbe ambao ninakuzungumzia leo sio tu tunachosema au ni upendo gani tunayohusika au wapi tunaenda. Lengo letu linapaswa kuwa juu ya kuijifahamu Wewe ni mmisionari kwa mama na baba yako. Wewe ni mmisionari kwa watoto wako. Wewe ni mmisionari kwa mwenzi wako. Wewe ni mmisionari kwa jirani yako.

Aina ya maisha ambayo unayoishi, aina ya moyo uliyo nayo, aina ya injili ambayo unayoishi - ikiwa ni nguvu, inayoingia ndani ya nafsi yako ili kukubadilisha kwa kiwango ambacho umebadilishwa - itakuwa kiwango cha ambayo unaweza kubadilisha na kubadilisha ulimwengu unaokuzunguka.