HII NI NIZAWADI YA AJABU KUTOKA KWA NEEMA

Gary Wilkerson

"Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu, wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu" (Waefeso 2:8-9, ESV).

Maisha yetu katika Kristo huanza kwa neema, inaendelea kwa neema, na itaisha kwa neema. Mara tunapofahamu jambo hili, maisha yetu yatakuwa na uhuru badala ya utumwa; kwa furaha badala ya uchovu; kwa furaha badala ya hofu. Kutumia muda mbele ya Mungu kutaonekana kama zawadi ya furaha kwa sababu tutakuja kuelewa kwamba sisi si watumishi tena lakini marafiki wa Yesu.

Kuelewa na kuzingatia zawadi hii ya ajabu ya neema haitoi jukumu letu la kujiadhibu wenyewe katika safari yetu pamoja naye, hata hivyo. Neema haikuja kutowa wajibu wetu wa kuendelea kutafuta uso wake.

Hapa ni ushauri wangu kwako: Usipuuze kuomba, lakini fanya hivyo kwa mafuta ya neema ya Mungu. Soma Biblia yako kwa neema au utakuja ukitokea nje kama aliehukumiwa na kuogopa badala ya kuangaziwa na kutiwa nguvu. Kwa nini? Kwa sababu ni kazi ya Mungu ya neema, ambayo inatuonyesha kutoweza kwetu wakati huo huo kutuwezesha sisi kutambua uwezo wake. Na wasiwasi kuacha kundi lako la uwajibikaji, hawa Wakristo wenzako wanaokupenda, kukuhimiza na kukutiya changamoto yote kwa wakati mmoja.

Neema inanyesha juu yetu kutoka kiti cha Bwana na neema ni namna inachora ulimwengu katika maisha yetu na ushuhuda wetu. Watu wanapoona neema ya Mungu juu yetu, watatambua kwamba mioyo yetu imeshinda kwa neema hiyo na siyo kwa kazi zetu.

Fungua moyo wako leo kwa neema ya Mungu, maisha yako yataonyesha wema wake kwa wale wote wanakuzunguka.