KWA UJASIRI KUKABILIANA NA KUSHINDWA KWETU
Adamu alipofanya dhambi, alijaribu kujificha kutoka kwa Mungu. Yona alipokataa kuhubiri Ninawi, woga wake ulimsukuma ndani ya bahari, akijaribu kuukimbia uwepo wa Bwana. Baada ya Petro kumkana Kristo, aliondoka na kulia kwa uchungu.
Adamu, Yona, na Petro walimkimbia Mungu, si kwa sababu walipoteza upendo wao kwake bali kwa sababu waliogopa kwamba Bwana alikuwa na hasira sana asiweze kuwahurumia.