YESU ANATUOMBEA

David Wilkerson (1931-2011)

Siku ya Pasaka, Yesu aligeuka kwa mwanafunzi mwenye ujasiri Petro na kufunua, "Petro, Shetani ametaka mimi kukupeleka kwa yeye ili aisumbue maisha yako."

"Bwana akasema, 'Simoni, Simoni! Tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; lakini nimekuombea wewe ili imani yako isipungue; nawe utakaporudi Kwangu, waimarishe ndugu zako." Naye akamwambia,"Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi nitayari kwenda gerezani au hata kifoni." Kisha akasema,"Nakwambia, Petro, jogoo hatawika leo kabla wewe hujanikana mara tatu ya kuwa hunijuwi" (Luka 22:31-34).

Petro alijisifu mbele ya wanafunzi wengine ya kuwa na imani isiyoshindwa , "Bwana, sitakuwa namashaka kamwe juu yako. Ninataka kufa kwanza. "Shetani alikuwa karibu kuanzisha shambulio lisilo la kawaida juu ya imani ya Petro. Kuchanganua inamaansha "kutingisha kwa ukali." Shika tu hili kwamba, shetani alitaka kutingisha misingi wa imani ya Petro kwa njia kali zaidi iwezekanavyo.

Petro alikuwa ametangaza imani yake katika uungu wa Yesu, akisema, "Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai" (Mathayo 16:16), hivyo imani yake ilikuwa ya kweli - ndiyo sababu hiyo Shetani alimfuata. Tunapokuwa katikati ya jaribio, ni vigumu kuona kwamba tuko katika moto kutokana na kutembea na Yesu. Lakini Petro alikuwa kuwa kama nguzo ya kanisa la Mungu, kwa kuanzisha injili ulimwenguni pote siku ya Pentekoste, na kuwa kuwa na hakika kwamba Shetani hangeacha hilo kutokea bila kupigana.

Yesu alijua shambuliyo la kishetani juu ya Petro lilikuwa li nalenga imani yake, hivyo alimwandaa mwanafunzi wake kwa kumwambia, "Nimekuombea." Fikiria – kwamba Yesu anakuombea! Wengi wetu tunaweza kupitia nyakati za kuchanganuliwa, lakini wachache wanaweza kufikiria mashambulizi ya Shetani kuwa makali sana kwamba tunaweza kujaribiwa kumkana Yesu. Ni faraja gani ya kujua kwamba hata kama tunapitia wakati wa imani isiyokamari, Yesu anatuombea, kwa kutuletea tena nguvu, wa kati tunapoludi, tuwe na ushahidi kwa wengine.