YESU ALISHIKIRIA LENGO LAKE

Gary Wilkerson

Kama wafuasi wa Kristo, tunapaswa kuwa makini kuanguka katika mtego unaopendwa na Shetani: kuingizwa katika hali mbaya ya utamaduni na ya kisiasa ambayo imezagaa katika dunia yetu. Kwa kuwa Shetani hufanya dunia kuwa hasira zaidi kwa Wakristo, yeye anajaribu kutufanya tukasirike na kulipiza kisasi. Kwa maneno mengine, anataka kuchukua nafasi ya amani yetu ndani ya Yesu kwa ugomvi, na kutufanya sisi kupinga mashambulizi ya mateso badala ya kuvumilia kwa ajili ya injili.

Kanisa halishiriki katika mechi ya ubao na ulimwengu wa kidunia, kusogeza vipande kwa makusudi na lengo moja katika akili: kushinda vita vya utamaduni. Lakini ikiwa hatujali, tunaweza kuingia katika "mchezo" na kuenea kwa chumvi na mwanga wote Kristo ametupatia ili tukamilishe malengo yake hapa duniani.

Huu utamaduni wa mapambano sio mpya. Fikiria mauaji ya kimbari ambayo yalifanyika huko Israeli wakati Yesu alizaliwa. "Sauti ilisikiwa Ramah . . . kilio na maombolezo mengi" (Mathayo 2:18). Yesu alikulia katika utamaduni ambapo hapakuwa na wavulana wa umri wake kwa sababu wote walikuwa wameuawa. Angeweza kukua akiwa na mawazo ya kulipiza kisasi, akifikiri, "Herode atawalipa yale aliyowafanyia ndugu zangu wote wa Kiyahudi. Siku moja nitamleta chini!"

Badala yake, wakati Yesu alikuwa kijana wa miaka thelathini, alianza kutangaza habari njema, kuwaponya wagonjwa, kufanya miujiza, hata kufufua wafu. Kwa kifupi, alikuwa akifanya biashara ya Baba yake. Alishikilia lengo lake! Hata wakati Mafarisayo walipomwambia kwamba Herode Antipa alitaka kumuwua (tazama Luka 13:31), aliwaambia wa ache mfalme afahamu kama ataendelea na kile alichokua anafanya. Alijua kwamba Herode alikuwa hatari lakini hakuwa na wasiwasi kufanya vita na yeye kwa sababu alikuwa na nia ya kutimiza kusudi lake la kuweka kila mtu huru!