WIMBO UNAOFAA, UPANDE USIOFAA

David Wilkerson (1931-2011)

Katika dhambi zote tunazoweza kufanya, kuwa namashaka ni kitu kimoja ambacho kinachukiwa sana na Mungu. Kwa mujibu wa Agano la Kale na Agano Jipya, mashaka yetu huhuzunisha Bwana. Tunaona mfano mkuu wa hii katika Israeli ya kale baada ya Mungu kuwaokoa watu wake kutoka kwa mkono wa Farao.

"Tumetenda dhambi pamoja na baba zetu, tumetenda maovu, tumefanya mabaya. Baba zetu katika Misri hawakufikiri matendo yako; hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, wakaasi kwenye bahari - bahari bahari ya shamu" (Zaburi 106:6-7).

Mwandishi anafanya hapa hutubu. Dhambi ambayo Israeli alifanya ilikuwa yenye mashaka kwao ya kuwa Mungu angeweza kuwaokoa, hata baada ya kufanya muujiza wa ajabu kwao katika Bahari ya Shamu. Inaonekana kuwa haikuwezekana kwamba watu hao hao walikuwa wana mashaka kuhusu uaminifu wa Mungu wakati walikabiliwa na magumu baadaye. Mtunga-zaburi anasema, kimsingi, "Je, unaweza kuamini? Bwana wetu alikuwa ametuokoa kutoka kwa adui, lakini sisi hatukumuamini."

Ilikuwa hadithi tofauti kabisa, hata hivyo, wakati Waisraeli walisimama upande wa ushindi wa bahari. Waliimba na kutembea walipokuwa wakiangalia jeshi kubwa la Misri likizama na kuangamia: "Maji yakawafunika waasi wao, hakusalia hata mmoja wao. Ndipo walipoyaamini maneno yake, waliimba sifa zake" (Zaburi 106:11-12).

Waisraeli waliimba wimbo sahihi - lakini waliimba kwa upande usiofaa wa bahari. Mtu yeyote anaweza kuimba na kufurahi wakati wana ushindi lakini wengi wetu ni kama Israeli, kushindwa kwa kusikitisha kabla ya kupitia ushindi.

Mungu alikuwa amethibitisha mwenyewe kwa watu wake Misri mara nyingi na ishara za ajabu na maajabu. Na Musa akajaribu kuwashawishi kuwa Bwana alikuwa akiwafanyia kazi, lakini bado walikuwa wakiwa na mashaka kwa Mungu, akifanya kazi zake kwa nguvu (Soma Kutoka sura ya 14 hadi 16.)

Hatuwezi kujenga imani yetu kwa miujiza pekee; badala, mara nyingi Roho Mtakatifu huimarisha imani yetu kwa Bwana kupitia majaribu yetu.