WATU WENYE NEEMA

David Wilkerson (1931-2011)

Mfalme Daudi mara nyingi alionyesha huzuni na mapambano yake: "Ningekuwa na mabawa kama njiwa! Ningerukia mabali na kustarehe. . . . Ningefanya haraka kuzikimbia" (Zaburi 55: 6 na 8). Wakati mwingine huzuni za Daudi zilimuendesha hadi kutoka machozi na anaonyesha wazi kwamba alikuwa na tamaa.

Kwa sababu tunaishi katika dunia iliyoanguka, sisi sote tunakabiliwa na siku za huzuni na mapambano. Jinsi gani, tunapaswa kupata neema ya kutusaidia wakati wetu wa mahitaji? Kutokana na ufafanuzi wa kiteolojia wa neema, hautatii wakati tunapokuwa katikati ya mgogoro. Tunahitaji msaada wa kweli sana wa Mungu tunapoumiza.

Mungu hutoa neema yake kwa njia ya mafunuo wakati wa majaribu yetu ambayo hatuwezi kamwe kuelewa katika nyakati zetu nzuri. Tunapata mifano ya hili katika Neno. Yohana alipokea ufunuo kutoka kwa Bwana wake, ambao imekuwa sehemu ya mwisho ya Maandiko: Kitabu cha Ufunuo. Katikati ya saa hiyo ya giza, mwanga wa Roho Mtakatifu ulikuja kwake na Yohana alimwona Yesu kama hajawahi kumwona kabla.

Mungu pia hutoa neema yake kwa njia ya watu wake, kwa kutumia watakatifu wake ili wawe njia za neema yake kwa wengine. Ninaita hili "watu wenye neema" na Paulo anaongea juu la hilo. "Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo" (Waefeso 4:7).

Na Petro anaandika, "Kila mmoja kwa kadirialivyoipokea karama, itumieni kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mabalimbali za Mungu" (1 Petro 4:10).

Fikiria juu ya maana ya kuwa msimamizi mwema, au mtoaji wa neema ya Mungu. Je! Wewe ni mtu kama huyo au unatumia muda wako kuomba tu kwa maumivu yako mwenyewe, huzuni na shida?

Wapendwa, mateso yako ya sasa yanazalisha kitu cha thamani katika maisha yako. Kama unapopokea neema yake kubwa, basi Bwana atakusaidia kuwa mtoaji wa neema. Jifunze maisha yake na ufurahi!