Watu Wa Mungu Hawata Aibika Katika Nyakati Za Janga Kuu

Nilipokuwa nikiliandaa neno hili, Gazeti la Wall Street Journal lilinakili kwamba Dunia nzima imefunikwa na wingu kuu la Uoga. Watu kutoka mataifa yote sasa wamebutwaa na matukio yalio ulimwenguni leo. Mara moja nilianza kuwaza kuhusu waumini wa hapa kwetu Times Square Church. Hawana uoga kama huwo. Ingawa tumemakinika na matokeo hayo, tuko pia na Furaha kuu. Nikaongozwa pale kwa Zaburi 37, ilioandikwa na Daudi: “BWANA anazifahamu siku za wanyofu, na urithi wao utadumu milele. Siku za maafa hawatanyauka, siku za njaa watafurahia kuwa na wingi wa vitu. Unabii wa ajabu kwa watu wa Mungu unaoendelea kutimizwa kati yetu hivi sasa. Kwa ufupi, Zaburi 37 inatueleza kwamba Mungu huinuka na kuhukumu Jamii ambazo dhambi zao zimeikera Mbingu. Daudi akatoa Unabii, “kwa maana nguvu za waovu zitavunjwa (Zaburi 37:17). Walakini, Zaburi hii iko pia na ahadi kuu kwa wenye haki walio mwamini Bwana. Kwanza kwaja nyakati ambapo Mungu hatastahimili tena uchoyo, tamaa na ufisadi ambazo waovu wametenda kwa maskini wasiojiweza. Unabii wa Daudi unanena kuhusu upotevu wa haraka wa nguvu za fedha. “Lakini waovu wataangamia: Adui za BWANA watatoweka kama uzuri wa mashamba, watatoweka, watatoweka kama moshi (Zaburi 37:20). Neno lanena kuhusu moto utakao choma mali na fedha zitakazo fifia kama moshi. Tafakari picha ya yale yalioitokea Uchumi wa Amerikani. Katika kipindi cha wiki mbili, zaidi ya takriban Trilioni 4 za dola za Amerikani zilififia. Sasa tunajulishwa kwamba trilioni zengine zitafifia pia kama moshi. Soko la hisa dunia nzima limeshikwa na butwaa na madalali wanalia wakipiga nduru. Sitaki kuifafanua sababu ya Mungu kuyakubali matukio haya, lakini nitasema hili: tunajua Mungu halali. Kunakuja kila mara kama vile asemavyo Isaya “Kwa sababu BWANA anayo siku ya kulipiza kisasi, mwaka wa malipo, siku ya kushindania shauri la Sayuni” (Isaya 34:8). “Mchana kutwa nimeinyoshea mikono yangu kwa watu wakaidi, wanaokwenda katika njia ambazo si nzuri, wafuatao mawazo yao wenyewe, taifa ambalo daima hunikasirisha machoni pangu, wakitoa dhabihu katika bustani na kufukiza uvumba juu ya madhabahu za matofali,… Tazama, jambo hili hubakia limeandikwa mbele zangu, sitanyamaza kimya bali nitalipiza kwa ukamilifu, nitalipiza mapajani mwao” (Isaya 65:2-3, 6)

Tunayaona katika Uchumi wetu sio tu Kulipiza kisasi kwa Mungu, bali ni kuimarishwa kwa Heshima na Utukufu wa Mungu. Hatasimama tu pale njia zake zinapoporwa na waovu. Ezekieli akaandika, “Wakati umewadia, siku imefika. Mnunuzi na sifurahi wala mwuzaji asihuzunike, kwa maana ghadhabu iko juu ya kundi lote...Wajapo piga tarumbeta na kuweka kila kitu tayari, hakuna hata mmoja atakayekwenda vitani, kwa maana ghadhabu yangu iko juu ya kundi lote (Ezekilei 7:12, 14). Katikati ya uovu Mungu ameipiga tarumbeta ya onyo, lakini onyo halikupewa maanani. Paulo aandika kuhusu nyakati hizi akisema, “Lakini yakupasa ufahamu jambo hili, kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari... Lakini watu waovu na wadanganyaji watazidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika (Timotheo wa kwanza 3: 1, 13). Tafakari rahani za nyumba walizoshindwa kulipa, na malipo yalipokuja waliachwa bila manyumba. Benki za sifa zilianguka kwa sababu ya uongo, lakini wakuu wa hizo Benki walijipea pesa za “Parachuti za dhahabu” (golden parachute) ya mamilioni ya pesa. Nasoma kuhusu wakuu hawa wakiandaa maamkuli, wakidensi usiku mzima wakinywa pombe wakiwa na ufahamu kamili kwamba kampuni zao zilikuwa zimefilisika. Waliburudika vivlivyo ingawa walijuwa wengi watapoteza nyumba zao. Ni wazi kabisa kwamba unabii umetimizwa: Sefania 1:9 “hukwepa kukanyaga kizingiti (ya maskini), ambao hujaza hekalu la miungu yao kwa jeuri na udanganyifu. Tulifikiri Mungu atavumulia wazimu huu kwa mda gain? kuchafuliwa kwa jina lake? Mungu ndiye analo neon la uamuzi kwa jambo hili, na asema, “Katika siku hiyo nitaadhibu wote” (Sefania 1:9). Kwa ufupi: “Nitawaibisha!” “Lakini panga zao zitachoma mioyo yao wenyewe, na pinde zao (mali na fedha) zitavunjwa (Zaburi 37:15). Ata hivi ninaponena na kuandika neno hili, mabilionea wawili wamepewa dhamana kwa sababu mali yao yote imepotea kwa usiku mmoja.

Wakati ule Mungu analipiza kisasi kwa waovu, atatunuka wale wenye haki wanao muamini.

Jameni, hili ndilo kiini cha maubiri yangu: “BWANA humtegemeza mwenye haki…Siku za maafa hawatanyauka (Zaburi 37:17, 19). Utauliza, “la maanisha nini hili neno kwa kweli? Lina maanisha: Mungu ni muaminifu sio tu kwa kulipiza kisasi lankini pia kwa kuweka ahadi zake. Daudi anasema hivi, “tazama kila mahali vile Mungu alitenda Neno lake, maonyo yake sasa yametimia na kuelezwa kwa habari zenu, matendo yake katika vyombo vya habari, kwani Mungu hatalitimiza Neno lake kuwahifadhi wateule? Tafakari tena: haijalishi lile litakalo tokea ulimwenguni – haijalishi habari zikiwa za kutisha kiwango gani, haijalishi kiwango cha kutetemeshwa kwa ulimwengu, vile uchumi utaanguka – watu wa Mungu hawata aibika kamwe. Kwa kweli, Mungu atatenda kulingana na Imani yetu kulitimiza Neno Lake kwetu. Ndio tutasumbuka, lakini tutanusurika wale tunaomuamini Bwana. Dunia haitaweza kusema eti Mungu wenu hakulitimiza Neno lake. Usidanganyike, tutakumbana na mambo ya ajabu yasiowezekana hapa mbeleni. Lakini Mungu wetu asema yeye ni Mungu wa yale yasiowezekana, anatenda muijiza pale hamna jibu la kibanadamu. Na tena, yeye aweka Sifa na Uvumo wake kwa mikono ya waumini, akituita tumkumbushe ahadi zake. Ungefikiri, “lakini Mungu aweza kulitetea jina lake mwenyewe. Hanihitaji mimi” la sivyo! Mungu amechagua watu wake wawe ushuhuda kwa dunia iliyo kiziwi iliyokosa kugusika na Mungu. Na anatuita tumkabili waziwazi katika yale aliyoahidi. Ona basi, kwa macho ya ulimwengu, Mungu kila mara yuko majaribuni. Wanaangalia kila mara tunapokumbwa na mambo yasiowezekana, wanasema, “huyu mtu huimba kuhusu vile Mungu hutengeza njia ya kumkomboa. Sasa wacha tuone kama Mungu wake atamjibu. Atafaulu kushinda haya ama ataishia kwa aibu? Wale wasioamini nyakati za Yesu walisema haswa vivyo hivyo pale Yesu alikuwa msalabani. “Sasa tutaona. Itakuwa kufufuka ama aibu?” Yesu hakuwa kiziwi asiweze kusikia uchokozi huwo. Lakini alijua jambo wale wasioamini hawakulijua. Baba Yake hatamuacha katika aibu. Mungu hangesita kumkomboa kwa ajili ya Jina Lake.

Kuna nyakati zikaazo kana kwamba Mungu ametoweka. – wakati ambapo watu wake wanaachwa kwa aibu na kuvunjika moyo – lakini hadithi nzima haija malizika. (Msalabani ilikuwa nyakati kama hii). Jambo linalotuponyoka wakati wa shida ni kwamba Heshima ya Mungu ikotaabani. Na wakati wote katika Bibilia tunawaona watu ambao Imani yao duni ilikwamilia kumuamini Mungu katika nyakati za janga kuu. Hawa watumishi, bila haya, walimuita Mungu atende jambo, kwa kuweka Heshima ya Bwana katika Kigingi, lakini wakimuamini kabisa kwamba ataleta Ukombozi.

1. Tafakari Mfano Wa Musa Pale Bahari Ya Shamu

Hili lilikuwa haliwezekani kwa nguvu za binadamu, waisraeli walikuwa mbioni kutoroka majeshi ya Misri, walipokuwa wamefungiwa na bahari pande moja na milima pande nyingine, Musa alimkabili Mungu katika Ahadi zake. Alikuwa amekwisha tabiri kwamba Mungu atawaongoza waisraeli mpaka Inchi ya Ahadi. Sasa Heshima ya Bwana ilikuwa katika Kigingi waziwazi. Nasikia ripoti zikirudi kuwa Farao amewatega waisraeli. Wote huko Misri walitazamia kwamba Farao atawarudisha waisraeli wakiwa na mapingu. Sherehe zingepangwa kufurahia ushindi wa Farao, pakiwa na vinyago vya dhahabu vikiinuliwa juu ya Mungu wa waisraeli. Musa alifanyaje kulingana na haya? Akitazama bahari ile kubwa mbele yake, alilia, “Songa mbele!” Musa aliamini kwamba Mungu atawatunza, aliamini neno la Bwana kwamba atawaongoza waisraeli mpaka Inchi ya Ahadi, Alikiri “Najua Mungu ni Muaminifu, nitatenda kulingana na Neno lake.” Tafakari matukio ya Imani hii. Kama bahari ya shamu haingefunguka kimiujiza, Musa angedhaniwa kuwa mjinga. Waisraeli wangerudi kwa utumwa, na Mungu hangewahi tena kuaminika. Lakini sote tunajuwa lililotendeka siku hiyo. Musa alinyoosha mkono wake, maji yalipasuka na kutawanyika na watu wakatembea kwa ardhi iliyo kauka. Mimi ninawaambia, hakuna yule anaye muamini Mungu atakaye aibika. Atatimiza kwa ahadi zake kwa ajili ya Jina Lake.

2. Tafakari Yoshua

Siku sita waisraeli walizunguka kuta za Yeriko, wakisema, “kuta hizi zitaporomoka.” Kwa wale waliokuwa humo Yeriko ndani, mambo hayo yalikuwa ni ujinga mtupu. Lazima walikuwa wamecheka mno. Mwishowe, siku ya saba, watu wa Mungu waliamuriwa wazunguke, si mara moja, lakini mara saba. Wakati huu, labda ata waisraeli wenyewe walisikia kama wajinga. Labda walifikiri, “haliku tokea lolote siku sita. Sasa ni kama tunapiga ngumi ukuta. Tutaaibika kama kuta hizi hazitaanguka. Walakini fikira kama hizi hazikumsumbua akili Yoshua. Yeye alinena, “Najua lile nililosikia kutoka kwa Bwana Mungu, najua pia kuwa Anaweza”. Alimkabili Mungu kwa ahadi zake, akiweka utukufu wa Mungu taabani. Tunajua lililotokea. “Watu walipiga nduru makasisi walipopiga mbiu: kisha...kuta za Yeriko ziliporomoka chini ndiposa Waisraeli wakaliingia mji nakuliteka nyara” (Yeshua 6: 20). Watu wa Mungu wanapomkabili katika Neno lake, Hawezi kuwaaibisha.

3. Tafakari watoto wakihibrania.

Danieli pamoja na wale Waibrania watatu walikataa kuabudu sanamu ya Nebukadneza futi 90 ya dhahabu. Walikaa ngumu hata walipohukumiwa kifo motoni. Mfalme muovu akinena, “Naye ni mungu yupi atakayeweza kuwaokoa ninyi, kutoka katika mkono wangu?” (Danieli 3:15), vijana hawa walimkabili Mungu kwa ahadi zake: “Ee Nebukadneza, hatuhitaji kujitetea wenyewe mbele zako kuhusu jambo hili, ikiwa tutatupwa ndani ya tanuru iwakayo moto, Mungu tunayemtumikia anaweza kutuokoa na moto, naye atatuokoa kutoka mkononi mwako, Ee mfalme. Lakini hata ikiwa hatatuokoa, Ee mfalme, tunataka ufahamu kwamba, hatutaitumikia miungu yako wala kuiabudu sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.’’ (Danieli 3: 16-18). Walikuwa na matumaini kuwa Mungu ataliheshimu Jina Lake, walikubali bila pingamizi kifo kwa moto. Viongozi Vigogo nchi nzima walikusanyika kuona Utengevu huu: Vibwana, Magavana, Mahakimu, Viongozi kutoka mikoa mbalimbali. Naye Nebukadneza akaamuru moto ishindikizwe mara saba kupita kawaida, ikawa moto zaidi mpaka ikawauwa hata wale waliokuwa wakiiasha. Mkusanyiko ulishtuka na kusema, “hawa vijana hawataishi, watakufa hata kabla ya kuingia pale motoni, hakuna mungu awezaye kuokoa kotoka kwa janga hili”. Kwa mara nyingine tena, Jina la Mungu lilikuwa taabani. Kama hangeingilia kati, jina lake lingedharauliwa dunia yote. Kwa kweli, Mungu hawaaibishi wale wanao muamini. Maandiko yanakili kwamba Yesu mwenyewe alitokezea motoni kuwalinda vijana wale na kuwafariji watumishi wake. Vijana wakihibrania walitoka motoni bila hata kunuka moshi.

4. Tafakari Mfalme Hezekia.

Maandiko yasema Hezekia alimcha Mungu: Alishikamana na BWANA kwa bidii wala hakuacha kumfuata (Wafalme wapili 18:6). Alipokuwa akiongoza, Yerusalemu ilipata kuzingirwa na Waashuru, waliokuwa vigogo wa vita zama hizo. Jeshi hili kuu lilikuwa tayari limekwisha teka nyara Samaria na miji ya Yudea, na sasa ilibaki Yerusalemu waliokuwa wamekwishazingira. Kapteni wao akawika, “tumewashinda nguvu miungu ya nchi zote, sasa munafikiri vipi kwamba huyu Mungu wenu atawaokoa?” Kwa mara nyingine, Mungu mwenyewe alikuwa taabani, Uaminifu wake ulijaribiwa mbele ya Milki yote, mbele ya maadui wa Israeli, na hata watu wa Mungu, je ingelikuaje Asingelitenda kitu? Waovu wangecheka na neno la Mungu lingekuwa tupu bila maana. Janga lilipokuwa likiendelea kuwa baya, Nabii Isaya alitazama haya yote. Alikwsha pokea Neno kutoka kwa Bwana Mungu, akaliamini kabisa. Kisha akamkabili Mungu kwa Neno hilo, ili kumuhushumu Mungu. Akaomba, “Mungu heshima yangu haijalishi kitu. Usipookoa watu wako mimi naweza kujificha mwituni, ni Jina lako lililotaabani. Kisha akimueleza kwa upole mfalme Hezekia amjibu Kapteni wa Ashuru: ‘‘Hataingia katika mji huu wala kupiga mshale hapa. Hatakuja mbele yake akiwa na ngao, wala kuweka jeshi kuuzunguka. Kwa njia ile aliyojia, atarudi, hataingia katika mji huu, asema BWANA. Nitaulinda mji huu na kuuokoa, kwa ajili yangu na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu.’’ (Wafalme wapili 19:32–34). Mungu hatakubali kamwe watu wake wanaomuamini waaibike, usiku huwo alitenda Miujiza ya ajabu. Maandiko yasema majeshi 185,000 ya Ashuru walikufa Kilingelinge, na kusababisha uoga mkubwa mpaka jeshi hili kuu la Ashuru likatimua mbio likihepa. Tena, Mungu alitetea watu wake kwa ajili ya Jina Lake.

5. Tafakari Petro na Yohana katika agano Jipya.

Wafuasi hawa wawili walipokuwa wakielekea Hekaluni kuomba, walikutna na maskini mlemavu toka kuzaliwa kwake. Petro na Yohana labda walimpita mtu huyu mara nyingi mbeleni, wakati huu walisimama. Watu waliokuwa sokoni wakamsikia Petro akisema, ‘‘Tutazame sisi..... Kwa jina la Yesu wa Nazareti simama, uende.’’(Matendo ya Mitume 3:4, 6). Petro alimwita Yesu atende jambo, Utukufu wa Mungu menyewe ukiwa taabani. Labda watu walisema, “jameni muubiri mjinga namna ganai huyu, anamuamuru kilema toka kuzaliwa asimame na kutembea.” Natumai watu hawa walikuwa tayari kucheka na kuwadhihaki Petro na Yohana. Walakini miguu ya kilema huyu ilianza kusonga, kuanzia kifundo cha mguu ikielekea juu mpaka mapajani. Akachuchumaa, akajiinua juu nakusimama. Watu sasa walipigwa na butwaa, kilema huyu aliyeponywa akarukaruka kwa furaha. Ingelikuwaje kama Mungu hangetenda jambo? Hilo halikumsumbua Petro, alimkabili Mungu kutenda jambo. Mungu hawezi kuwaaibisha wale waliomuamini.

Sisi leo pia tunaweka Heshima na Utukufu wa Mungu taabani.

Tafakari matukio haya katika Bibilia. Katika kila hadithi, Sababu zote zilizo mfanya Kristo kuja na Kufa msalabani zilikuwa taabani. Walakini, katika Agano la Kale na Jipya, mipango na maono ya Mungu ilisimama na watu wa Mungu waliimarishwa. Katika hali zote, Mungu alitazamia watoto wake sio kumuamini tu bali kuamini pia uwezo wal´ke kutenda miujiza. Je, Mungu asitarajia haya kwetu? Tazamia Ushuda tuliompa Mungu, tumesema atakimu mahitaji yetu, tukamwita Yehova Jire. Tumenena ahadi zake za kukimu watoto wake. Sasa tena Heshima yake na Utukufu wake uko taabani. Tukimkabili atende, Mungu atuahidi: “Lakini kwa ajili ya jina langu nikafanya kile ambacho kitalifanya jina langu lisitiwe unajisi machoni mwa mataifa ambao mbele yao nilikuwa nimewatoa Waisraeli” (Ezekieli 20:14). Bwana asema, “Nilipowaokoa waisraeli sikuwa nimejificha mahali, nilitenda miujiza waziwazi diniani. Sasa nataka kutenda haya katika kizazi chenu”. Wapendwa, je unapitia janga ambalo hujamkabili Mungu? Je unaitwa uiweka imani yako kwa mambo usioweza kupanga? Umeafikia kwamba “ni Muujiza tu kutoka kwa Mungu itakayo niokowa sasa?” labda hatutaweza kujua vile Mungu atatenda miujiza yake; hamna yule alijua katika Biblia yote. Lakini twajua haya; malaika mmoja tu aweza kutorosha majeshi 185,000. Mungu hawezi kuaibisha watu wake!

Kwa sasa, anatuambia yale aliyowaambia Waisraeli, “Niliwaita kutoka kwa dhambi zenu. Nimewaimarisha wazi mbele ya wale walio karibu nanyi ili nilitukuze Jina Langu. Nimimi niliye kuita utoke nje, nanitakuokoa kutoka kwa waovu kwa ajili yangu mwenyewe.” Utatembea basi kwa yale unayo ubiri na kuyamini? Utamkabili Mungu kwa Neno Lake ili Jina Lake litukuzwe mbele ya Mataifa? Naomba tuchukuw Ombi la Daudi la Nyakati kama hizi: “Lakini Wewe, Ee BWANA, Mwenyezi, unitendee wema kwa ajili ya jina lako, uniokoe kwa wema wako: (Zaburi 109:21). Mungu hatawahi kuwaaibisha wale wanao muamini. Atalitimiza Neno lake kwa ajili ya Utukufu wake.

---
Maandiko yamenakiliwa kutoka kwa IBS-STL Global translation http://www.ibs.org/bibles/swahili/index.php)