WATU AMBAO MUNGU ANAJIVUNIA

Gary Wilkerson

"Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu" (1 Petro 4:17). Mungu anataka kanisa safi ili tuweze kuwa watu ambao anatamani sana kwamba sisi tuwe safi na wasioambukizwa na ulimwengu. Anataka kufanya kazi ya kina ndani yetu ili kutusaidia na kutufanya kuwa watakatifu, ni Mungu wa ajabu tunayemtumikia.

Hukumu ya neno ina maana zaidi ya moja. Inaweza kutafsiriwa kama ghadhabu ya Mungu, ambayo ni kwa wale wasiomtii Bwana, lakini hukumu inayofika kwa nyumba ya Mungu sio ghadhabu ya Mungu; badala yake, ni kama moto wa kusafisha. Inatuleta mahali ambako maisha yetu yanatiwa kwenye msitali pamoja na kile anacho kwa ajili yetu.

Sura nzima ya nne ya 1 Petro inaelezea wazo la maisha yetu gisi yanayoonekana wakati hukumu ya Mungu, yenye upendo, inakuja na kututakasa. Anatupeleka mahali patakatifu: "Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi" (4:1). Kujihami mwenyewe husema juu ya kutembea ndani ya moto wa Roho Mtakatifu ili tuweze kuwa watu ambao wanasema ndiyo mipango yake kwetu.

Katika 1 Petro 4:8, Petro anasema tunapaswa "kupendana sana, kwa maana 'upendo utafunika dhambi nyingi.'" Tunaona kwamba utakatifu sio tu yenye tunayofanya, ni jinsi tunavyoishi . Aina kubwa ya utakatifu ni upendo; Kwa kweli, "yeye anayependa mwingine ametimiza sheria" (Warumi 13:8).

Utakatifu, moto wa kusafisha, hukumu ya haki ya Mungu - yote haya yatakuwa kwenye msingi wa moyo wako na kukubadilisha. Na aina hiyo ya hukumu itawafanya kuraramika sana kwa kusema, "Bwana Yesu, kuja!"