WALIKUWA HURU NDANI YA TANURU!

David Wilkerson (1931-2011)

Sisi sote tunajua hadithi vizuri. Mfalme Nebukadneza, mtawala wa Babloni, aliita kila kiongozi kutoka katika ufalme wake wa mbali ili kukusanyika pamoja ili waheshimu miungu ya uongo. Mfalme alijenga sanamu kubwa, dhahabu na kujaza viongozi wenye kuvaa mavazi ya kuvutia – wakuu wa majimbo, wana wa mfalme, mahakimu na maafisa wa majimbo - pamoja na watu wote wa nchi walipaswa kuzingatia amri ya mfalme na kuinama mbele ya sanamu. Je! Na kama hawangerifanya hivo? Ilikuwa ni hukumu ya papo hapo ya kifo.

Shadraki, Meshaki na Abednego, wanaume watatu wa Kiebrania wa kipekee, walikuwa wamechukuliwa mateka na kuletwa ikulu, waliyofundishwa kwa lugha hiyo, na kuteuliwa kuwa viongozi katika serikali. Wakati mfalme Nebukadneza aliamuru kila mtu ainame mbele ya mungu wake wa uongo, vijana hawa walikataa. Viongozi wenye wivu mara moja walitowa ripoti kwa mfalme aliyepiga ghadhabu na kuwapeleka mbele yake. Alipiga kelele, "Je! Ni aje mwanachama yeyote wa serikali yangu anaweza kusubutu akasimama kwa kunipinga kwa kutotii!"

Katika siku hizo, waasi wa amri za mfalme walikuwa wanatupwa kwenye tanuri ya moto. Mfalme aliamuru tanuru ifanyike mara saba zaidi kuliko kawaida na akatoa changamoto kwa Shadraki, Meshaki na Abednego tena: "Nani atakayowaokoa kutoka mikononi mwangu?" Wakamjibu, "Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa kutoka kwa tanuru ile iwakayo moto; atatuokoa kuto mkono wako, Ee mfalme" (Danieli 3:17).

Unaweza kuwa na hakika kwamba hawa vijana watatu wangeweza kuhisi joto la tanuru na nina hakika hawangekubali kufa. Lakini walikuwa na imani ya ajabu iliyowekwa ndani ya mioyo yao na Roho Mtakatifu tena walikuwa mashujaa, wasioachilia. Mfalme na wanachama wa ufalme waliangalia wakati wirikua wanafunga wanaume hao na kutupwa ndani ya tanuru.

Fikiria mshangao wao wakati waliwaona wanaume wakitembea juu ya makaa - na mtu wa nne katikati ya moto! Vifungo vyao vikaanguka na wakainua mikono yao, wakimsifu Mungu! Yesu alikuwa pamoja nao katika shida yao na wakatoka nje ya moto kama ushuhuda kwa wote.