Wako Wapi Wale Wengine Tisa?

Tafakari tukio hili kutoka Luka 17: Yesu alikuwa akielekea Yerusalemu wakati kusulubiwa kwake kulikuwa karibu. Alipokuwa akipita katikati ya Samaria na Galilea, alikaribia kijiji fulani ambapo kulikuwemo Wakoma kumi nje ya kijiji hiki waliokuwa wamepiga kambi kwa uchungu na pia aibu kuu. Kwa kweli, tisa kati ya hawa Wakoma kuni walikuwa wayahudi na mmoja aklikua Msamaria. Kumbuka kwamba, Wayahudi wa siku hizo walikuwa hawawezi hata kuwagusa Wasamaria wacha hata kuishi nao. Yaonekana shida ya ukoma iliyowakumba watu hawa iliwalazimu kubeba pamoja shida hii ya Ukoma.

Kwa wale ambao wamesomea ugonjwa huu, angalau unaweza kutafakari hali duni ya watu hawa. Yale tuyaonayo kila siku hapa New York City tayari ni mbaya mno. Hapa “41st Street”, karibu na Lincoln Tunnel, majengo duni ya makaratasi yamepangwa njiani, utaona hapo godoro chafu zilizooza, matambara na takataka zimerundikwa juu ya majengo haya. Ni kama mji mdogo ulio jaa chawa, panya, madawa ya kulevya, pombe, Ukimwi na magonjwa mengine pamoja na vita bila mkomo. Walakini, niamini nikikueleza kwamba majengo haya duni ya New York ni Ikulu tukilinganisha na pale Wakoma wale walikuwa wamepiga kambi nyakati zile Yesu alipokutana nao. Watu hawa hawakuwa na usaidizi wa vilema kutoka kwa serikali yeyote, hawakuwa na mpango wa kula bure, hospitali wala malipo ya maskini. Walikuwa wametengwa kabisa kutoka kwa jamii. Walikuwa maskini waliotupwa nje – waliolazimishwa kuishi nje ya kijiji. Wakoma walitakiwa kisheria kukaa futi 200-300 mbali na watu wengine. Watu wanapopita karibu nao, ilitakikana wapige mbiu wakisema, “Wachafu, Wachafu!” Kutokana na mda wa Ukoma wao, wengi wa watu hawa walikuwa wamepoteza vidole vya mkono au mguu, masikio, meno, mikono na pua. Ngozi zao zilikuwa zimeoza – na mnuko mahala hapo ulikuwa wakushtua mno. Watu hawa waliombaa, kubambanya na kula chakula ambayo watu wengine wangekosa hata kuiangalia. Inawezekana watu hawa waliishi mapipani. Na tena jambo lakuwasikitisha mno ni kukumbuka wapendwa walioacha nyumbani walipohukumiwa na Kasisi kwamba wao ni Wakoma. Walipoteza mabibi wapendwa, watoto wenye furaha, makao, kazi na utumishi wa aina yeyote ile. Inawezana kwamba wengine walikuwa labda Wayahudi waaminifu waliofuata maagizo ya dini kikamilifu. Lakini sasa walikuwa wamepiga kambi nje ya kijiji wakiishi maisha ya upweke yenye aibu na majonzi chungu nzima.

Maandiko yatuonesha kwamba Mkoma ni mfano wa mtenda dhambi anaishi kwa aibu – aliyeporwa na kumalizwa na majiraha ya dhambi. Katika Ibada zetu hapa Times Sqaure Church mara nyingi mistari mitatu ya viti hapa mbele hukaliwa na watu waliokuwa “Wakoma” hapo zamani. Vijana wadogo kutoka Timothy House, walikuwa watumiaji wa madawa ya kulevya na walevi wa kupindukia. Ukoma wa dhambi uliwadai wengi wao yote waliokuwa nayo. Bibi, watototo, kazi, heshima, afya, akili timamu na usafi. Wengi waliishia wakiwa bila makao, wasiojiweza na wapotevu. Sijui vile hawa Wakoma wakumi walisikia kuhusu Yesu. Labda Mkoma mmoja shujaa wa Kutangatanga alipitia hapo na kuwaeleza kuhusu yale makuu Yesu alikuwa amewatendea Wakoma kutoka miji mingine. Hata hivyo, walipata kujua kuhusu Yesu, na kwamba Yesu atapitia hapo karibu na wao na walikuwa wakimgojea kwa hamu mno. Jaribu kutafari haya. Wamekaa pale, karibu na barabra kama iwezekanavyo, lakini futi 200 hadi 300 mbali na barabara inayo pitia watu. Wamepiga kambi usiku mzima. Jameni jambo la kusikitisha kweli kuwaona watu hawa! Wakoma kumi wanukao wenye ngozi iliyooza, wakielekea kufa, wameshikana wakiinuana wakingojea tu pale Yesu atapitia barabarani. Mara nyingi nimewaza moyoni, Wakoma hawa walimuona Yesu na wanafunzi wake wakija pale barabarani, wakaanza kupeperusha mikono yao iliyopooza. Je, inaweza kuwa walikuwa wakioneshana pande za mwili zilizokatika? Au walikuwa wakipeperusha matambara chafu zilizo raruka? Sijui walimwita vipi Bwana Yesu. Lakini Yesu alipokuwa karibu vilivyo, walipaza sauti wakilia, “Yesu, Bwana, tuhurumie!’’. Walikuwa hawa ombi pesa, au Ahera wakifa. Walikuwa wanalilia Huruma. Ni kana kwamba walikuwa wakiomba – “Yesu – itawezekanaje ukumbane na jambo la kusikitisha kama hili bila kuwa na Huruma? Utawezaje kutunyima jibu? Niko na hakika, Yesu hakusita wale kuangalia kando hata kidogo. Aliwaangalia nyusoni mwao na kwa Huruma na Upendo mwingi akasema, "Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani" (Luka17:14).

Unaweza kufikiria Wakoma hawa waliwaza nini? Turudi kwa Makuhani? Kwanini? Wao ndiwo waliotutazama na kunena kwamba sisi tuwachafu! Walitufurusha nje ya Mji. Sisi wote kumi tukijipeleka mbele ya mlango wake, atatutazama mara moja tu na kukashifu ufedhuli wetu. Hakuna yule ashawahi kupona Ukoma. Atafikiri tumekuwa wazimu. Lakini naamini kwamba Wakoma wote kumi walihisi mtiririko wa Maisha, Afya na Nguvu! Mmoja kausongesha mkono ambao hakuweza kitambo kuusongesha, mwengine akisikia Maisha yakibubujika moyoni mwake – na akaanza kurukaruka juu chini! Mmoja baada mwengine, wakaangalia mikono yao, nyuso zao – na ngozi zilizo parara na kuoza ikaanza kugeuka. Ngozi yenye afya ikaanza kufunika viungo vyao, nyuso zao – walikuwa wanapona!

Je unakumbuka wakati Yesu alipokuhurumia wewe? Vile ulihisi usafi na maisha mapya! Ulipiga mbiu kwa sababu ulihisi Nguvu za Yesu zinazo safisha? Ulihisi maisha mapya ndani yako? Watu hawa walilazimika kuhisi maisha hayo mapya! Uwe na hakika kwamba msisimko maradufu wa furaha ulisambazwa kati ya watu hawa, na wakalipuka na kelele za furaha! Ngozi iliyopara na kuoza ilikuwa inapona. Na pale kulikuwa na vidonda, kulifunikwa na ngozi mpya yenya afya mno!

Katika Luka 5:14, Yesu alimueleza mkoma mwengine, “nenda ukajioneshe kwa Kuhani, na utoe sadaka ya Utakaso kama vile Musa alivyo waamuru, iwe kama Ushahidi kwao” (Luka 5:14). Hakuna Mkoma angewekza mara moja kurudi nyumbani kwake, Kanisani au kwa majukumu na haki za Agano. Ilimlazimu kwanza afanya mambo fulani. Kwanza, ni lazima atajwe kuwa Msafi na Kuhani – na jambo hili lilihitaji mipangilio ya sherehe za kidini za karibu siku nane. Ililazimika anyolewe kipara kabisa, aoshwe na kuchunguzwa kikamilifu. Kisha ifwatwe na utoaji wa sadaka, kunyunyiziwa kwa damu na mafuta, kupakwa mafuta, utoaji wa dhabihu. Baada ya haya yote, ilimlazimu kungoja tena siku nane kabla hajajumuishwa kwa Familia yake na kurudia mipangilio na haki za kidini. Kwa ujumla, siku kumi na sita zilihitajika kwa mipangilio na sherehe hizi za utakaso za ajabu mno! Sherehe hizi za kidini ni ishara – ishara ambazo hutumiwa kueleza watu kuhusu Utukufu wa Mwokozi Yesu. Yote haya yamenakiliwa kwa Walawi 14: na haya ndio Wakoma wale kumi walirudi kutimiza mjini.

Katika muda huwo, labda Yesu na wanafunzi wake walikuwa wameshakula chakula cha mchana, na walikuwa wameanza safari tena wakiwa mbali na kijiji hiki. Muda si muda wakasikia kelele nyuma yao, walipogeuka na kuangalia nyuma, walimuona mtu akitimuwa mbio akija kwao – akipiga nduru na kupeperusha mikono yake! Mmoja wa hao wanafunzi akasema, “ni mmoja wa wale Wakoma kumi kutoka kwa kile kijiji”. Na alipokuwa akikaribia, wakamsikia akipaza sauti, Utukufu – Utukufu kwa Yesu! Usifiwe Bwana! Ilikuwa ni yule Msamaria mmoja! Alipomfikia Yesu, alijiangusha miguuni mwa Yesu akalala kifudifudi na kulipuka tena kwa sifa na shukurani. Kutoka ndani ya moyo wake akamsujudu Yesu mwana wa Mungu aliye Hai. “wewe ni Mungu, hungeweza kufanya hivi kama hungekuwa mwana wa Mungu. Sifu Mungu, Utukufu kwa Mungu!

Yesu alimtazama nakumwambia, “Je,hawakuponywa wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? (Luke 17:17). Alikuwa anauliza, “kwanini wewe tu? Wako wapi wale rafiki zako niliyoponya?” wapendwa, hilo ndilo swali Yesu auliza hata leo! Kati ya wale maelfu na maelfu aliyowaponya na kuwaweka huru, ni Masalia tu wanaovutiwa kwake! Wako wapi wale wengine basi? Nitakueleza walipo – wako pahali sawa na wale Wakoma walioponywa: wamepotea ndani ya kanisa – wamemezwa na dini!. Ninaamini takwimu za Bibilia, na kama takwimu za hadithi hii ni sahihi, basi asilimia 90 ya wale wanaoguswa na Yesu hurudi kwa kanisa lilolokufa na kukauka mno! Hawamfikii Yesu – kwa sababu wamepotea katika dini! Wakoma hawa tisa walikuwa na haraka ya kurudi kwa maisha yao waliyokuwa wameacha mbeleni. Walisema, “lazima nirudi kwa mke wangu na jamii yangu. Nataka heshima yangu irudi. Nataka kurudi Sinagogu niendelee kusoma kuhusu kuja kwa Mwokozi wetu!”. Labda utasema, ni nini kibaya hapo? Si mtu ameamuriwa kuilisha jamii yake? Na Daudi pia aongea kuhusu kuwaza kwa undani mambo ya Mungu? Wakristo si pia wanastahili kuwa na motisha ya kufanya kazi kwa bidii? – kufanya vile hawa Wakoma walifanya? Kwani Yesu hakuwaambia waende kwa Kuhani? Ndio, yote hayo ni kweli – lakini yote huwa bure kabisa kama kwanza hatuta chukuwa fursa kumjua Yesu kibinafsi!

“Enendeni...kwa Kuhani....iwe kama ushahidi kwao” (Luka 5:14). Kwa miaka mingi ijayo, Wakoma hawa watamiliki Ushahidi wa ajabu kweli. Wangeweza kwa maisha yao yote kueleza tu vile Yesu alitenda. “Nilikuwa wakati mmoja Mkoma, mwenye upweke bila matumaini – mchafu, mpotevu, nikielekea kufa. Lakini Yesu alikuja na kunitakasa. Nimeponywa sasa ya timia miaka ishirini na tano – sifu Jina la Bwana.” Yote hayo yaonekana bora, laniki shida ni kuongea kumuhusu mtu wasiyemjua kamwe – wakitoa Ushuhuda wa Nguvu za Mwokozi ambaye hawaelewi kitu kumuhusu. Wanamtaja akiwa mbali. Wangekueleza umbo Lake, vile anaongea, vile atembeavyo – lakini hawakusonga karibu Naye wala karibu na moyo Wake!

Jambo linalonisikitisha sana katika miaka yote yangu ya huduma ni kushuhudia kuchoka kwa wale waliokuwa watumizi wa dawa za kulevya na walevi waliyo kombolewa kimuijiza kutoka kwa maisha ya dhmabi mbaya na uhalifu. Wengi wao waliitwa na Mungu kuuburi Injili, lakini Makanisa na Wachungaji Merikani kwote hawakukoma kuwaita watoe ushuda wao. Walibembelezwa kutoa siri za maisha yao ya kitambo. Na baada ya miaka kadhaa, wengi wa watu hawa washuhudia jambo moja tu. “miaka kumi na tano iliyopita nilikuwa Kuwadi wa malaya. Nimeishi na makahaba na nimefungwa jela mara ishirini. Siku moja mtu akanieleza kuhusu Yesu – na nikatakaswa na kufanywa Upya.” Wapendwa, mamia ya watu hawa sasa wame choka na kuanguka kutoka kwa wokovu kana kwamba meli zao zimegonga mwamba. Hawana hata utu wa Kristo, hawana uhusiano na Mungu, kwa sababu wanaishi kwa ushuhuda mmoja tu wa kitambo mno. Hawakurudi kwa Yesu, hawakuweza kumjua.

Watu wengi uniuliza, kwa nini wale wanao okoka katika kazi zetu za Uinjilisti wasitoa ushuhuda wao kila wiki hapa Times Sqaure Church? Kwa kweli hawa wanaume na wanawake wanaushuhuda wa ajabu kweli ambazo hujawahi kusikia. Lakini sisi tunawatazamia mema na zaidi kuliko tu ushuhuda mmoja mzee uliyoisha ladha. Tunataka waendelee mbele na Yesu – waweze kusimama na kueleza mapya kuhusu matembezi yao ya kila siku na Yesu, kuhusu yale mambo Yesu amewafanyia leo! Tunataka wampate Yesu Kristo kwa wingi kabisa!

Watu wengine ni kukataa wamekataa kutembea na Yesu. Wanapendelea dini aliyokufa! Wanafurahia msisimka na utamaduni wa ibada za kidini. Jameni ukifikiri tu vile Wakoma wale tisa walihisi walipokuwa katika mikakati ya utakaso! Ilikuwa ni sherehe za ajabu mno! Kwanza, Kuhani alichukua ndege wawili, akaua mmoja juu ya kibakuli cha maji “ya uzima” na kuwachilia damu ya ndege huyo kutiririka ndani ya maji. Kisha akafunga Hisopo kwa mbao ya mti wa Mwerezi (karibu inchi kumi na sita) na kuifunga kwa yule ndege aliye hai akitumia pamba nyukundu. Mabawa na mkia wa Ndege huyu zilitumbikizwa ndani ya damu iliyochanganyika na Maji. Damu hiyo pia ilinyunyiziwa Mkoma aliyepona kwa kipaji chake na kwa viwiko vyake mara saba. Kisha ndege huyo aliyehai aliachiliwa kupeperuka wazi uwanjani. Baadaye, Mkoma huyo aliyepona aliosha nguo zake na kunyoa nywele zake ata pia kuoga kwa utaratibu na kisha alirudi mjini kwa kitengo cha siku saba. Siku ya nane, alirudi kwa Kuhani na wana kondoo wawili wakiume na kondoo mmoja wa kike asiyekuwa na mawaa. Alileta pia galoni 2.8 za unga na painti moja ya mafuta kama sadaka ya kuvunja sheria, sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa. Kuhani alichukua mafuta yale na kuyapaka kwa viganja vyake, na kunyunyiza mara saba chini kwa ardhi. Kisha alichukua damu ya mwana kondoo, alimgusa nayo Mkoma aliyepona kwa ndewe la sikio lake la kulia, gumba lake la kulia la mkono na mguu pia. Kisha kuhani alichukua mafuta na kumpaka tena sehemu hizi tatu, mafuta iliyobaki alimmwagia kichwani mwake.

Ilikuwa sherehe za ajabu kweli – Wakoma wale waliopona walijihisi wanadini vilivyo. Sherehe hizi za kidini zilisimamia mambo ya undani sana kiroho – Upako, Utakaso na damu ya mwana kondoo. Walakini, yote hayo yalikuwa ni mfano wa mauti!, Wakoma walitoka kuguswa na Yesu na kuelekea dini ya mauti iliyojaa mila na desturi. Kwa kweli walikuwa wamerudishiwa heshima zao, walikuwa wamerudi kwa maisha yao kanisani, walipata tena baraka za mali, lakini hawakupata kumjua Yesu! Je utauliza, kwanini Yesu aliwarudisha wafanya mambo haya ya kidini? Mimi ninaamini Kristo aliwatuma kwa Kuhani akiwa na matumaini kwamba Wakoma wale watakuwa na kiu ya kutambua maana ya Undani ya desturi hizi za kidini. “Maji yanayotiririka” – si Yesu alisema kuwa yeye mwenyewe ndiye Maji ya Uzima? Unyunyizaji wa damu – si Yesu alisema Damu yake itamwagwa, kwamba yeye Atasulubiwa? Mwana kondoo kuchinjwa – hiyo inamaanisha nini? Tazameni, hakuna Kuhani Israeli yote angeweza kuwaeleza Wakoma hawa maana ya desturi hizo za kidini. Walifanya tu kama mazoea. Yesu alitazamia kwamba Wakoma hawa watamrudia awafunze mwenyewe. Walipomlilia hapo kandokando ya Barabara, “Bwana tuhurumie!” walitumia neno lililosawa na kusema “Jemedari, Mwalimu!” walijua alikuwa na Ukweli wote – lakini hawakua na kiu ya Ukweli huwo.

Hawa Wakoma kumi wanawakilisha maelfu ya watu leo wanao kaa Kanisani wanaosikiliza wachungaji ambao wanaubiri mambo wasiyoyaelewa. Maubiri yaliyokauka, yanayopekecha – yaloyokosa maisha! Lakini sasa najua kuna kizuri kimoja kimeletwa na hali hii, watu wamechoshwa, watu wameanza kusema, “Yesu hakuniokoa nikaye hapa nikauke, chini ya mchungaji ambaye anafanya kazi kama desturi tu ya kidini. Nipe Ukweli! Nipe Kristo!

Ni kwanini kwamba katika kila uzazi kuna wale wanao mkimbilia Yesu kwa Shauku na Shukrani kuu? Kanini Mungu anakuwa kila mara na yule mmoja anayeacha yote na kurudi kumsifu na kumuabudu Kristo? – wengine asilimia 98 wakiendelea tu na desturi za kidini? Naamini Msamaria alimrudia Yesu kwa sababu hakuwa amefungwa na utamaduni wa wayahudi. Lakini Msamaria alipoona mikakati na desturi ya kidini alilia “La hapana! alishuhudia ufananisho feki uliokuwa na wale makuhani na waumini. Aliona wafarisayo wakiibia wajane na kuchukua nyumba zao. Aliona Makuhani wakipeana rushwna na kula rushwa. Aliona sinagogu lililojaa wafanyi biashara wakigeuza pesa, waliogeuza nyumba ya Mungu kuwa ukumbi wa wezi! Akaona waandishi wakitengeza sheria ya kufwatwa na watu wengine ingali wao hawakuinia hata kidole kimoja kizifuata! Aliona nyuso zilisopakwa “chokaa”, nyuso za uongo na zinazokosa usawa. Na akajiambia, “hapa naona vipofu wakiongoza vipofu – hapa hapanifai mimi, nataka ile Halisi!

Alipokuwa akielekea kule kijijini na wale tisa – kurudi kwa makuhani, kurudi kanisani, kwa jamii, heshima na maisha mazuri – alisimama na kufikiri: “ngoja kidogo” nakumbuka vile ilikuwa nilipokuwa na kila kitu – pesa, fahari, usalama. Jameni nilikuwa Mtule! Rafiki zangu wa dhati walinikana nilipowaeleza kwamba labda niko na Ukoma. Nilikuwa Upweke! – Mfungwa katika dhambi, aliyejaa chuki na uchungu moyoni, ilikuwa kama kuzimu! Kwanini nirudiye maisha hayo? Kisha kitu kilianza kumchoma moyoni: “hebu niangalie mimi – Nimekuwa msafi sasa, Yesu ameniponya! Kanisa litangoja kwanza – familia itangoja kwanza. Mimi naenda kwa Yesu! Nataka kumjua yule aliyeniponya! Aliafikia azimio ambalo Wasalia wengi hufikia: “hamna lolote kule nje ninalolitaka, yote ni bure! Mimi naenda kwa Yesu – Yeye ndiye atakuwa Ukweli wangu!”

Mkoma huyu Msalia hangeweza kukoma kulia, “Utukufu! Sifa zilibubujika kutoka ndani ya Nafsi yake. Ninaamini kuwa yeyete amuabuduye Kristo kama huyu mtu – akijilaza kufudifudi miguuni mwake, akilia bila kujizuia – huyo atakuwa ameamua kabisa kutomwacha Yesu tena! Moyoni mwake asema, “nitaenda kwa nani mwenigine? Yeye anayo maneno ya Uzima wa Milele! Tafakiri mtu huyu anapotokea kila mahali Yesu anapofunza, wakati Kristo akiwa kando ya mlima, ama kando ya bahari, hapo yupo yule Mkoma aliyetakaswa akiwika: “nakupenda Yesu! Utukufu kwa Mungu! Sifa Kwako!” Ninamuona mtu huyo Yesu alipokuwa akipaa Mbunguni akilia, “Yesu nichukue twende nawe!” Napenda kufikiri kuwa alikuwa katika chumba kile cha juu wakati wa Pentekosti akimsifu Mungu – akiwa amejazwa na Roho Mtakatifu!

Ukweli ni Kwamba, sisi tumepewa kitu ambacho huyu Mkoma mwenye shukurani hakuwa nacho. Uweza mkuu unao zidi nguvu zote zijulikanazo hapa ulimwenguni. Kila Januari, sisi Waamerika umtuza Rais kwa kiti kiitwacho, “Mamlaka yenye nguvu zaidi duniia nzima!” Sahihi yake ni sheria. Ana mamlaka juu ya Jeshi la nguvu zaidi duniani. Inambidi tu afinye tu kitufe kuleta maafa dunia nzima. Walakini, nguvu za Rais huyu, hazikaribiiani kamwe na Nguvu zile Yesu ametupatia mimi na wewe! Tazama tuko na fursa isiyo na kipimo kusongelea na kuja mbele za Muumba, Mungu Aliyehai – na pia Yeye kuja kwetu! "Kwa hiyo, ndugu zangu, kwa kuwa tunao ujasiri wa kupaingia Patakatifu pa Patakatifu kwa damu ya Yesu, kwa njia mpya iliyo hai tuliyofunguliwa kwa ajili yetu kupitia kwenye lile pazia, yaani, mwili Wake, basi kwa kuwa tunaye kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu, sisi na tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu kwa imani timilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyizwa damu ya Kisto na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya nayo miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi. " (Waebrania 10:19-22).

Huyu Mkoma hakuwa na Nguvu hizi zilizokuja pale pazia ya Hekalu ilipopasuliwa mara mbili. Mambo haya yalipotendeka, ilimaananisha kwamba binadam angeweza kuingia ndani na Mungu pia angeweza kutoka nje – kukutana nasi! Neno “Ujuba” hapa lina maanisha “Kuwa na Uwazi uliofichuliwa waziwazi”. Wapendwa, “Uwazi” huwo ni kwa sababu ya Shetani! Inamaana ya kwamba tunaweza kukemea mapepo yeyote kutoka kuzimu tukisema, “Nina Haki katika Damu ya Yesu kuingia katika Uwepo wa Mungu na kuongea Naye! – naye Mungu kuongea nami! Je unaamini kuwa uko na Haki hii? – kwamba Mungu yu tayari kutoka ili kukutana nawe? Basi tumsongelee Mungu na moyo uliojaa Imani! Hatuji kwa damu ya ndege, mbuzi au Ndume – lakini kwa Damu ya Bwana wetu Yesu! “Hakuingia kwa njia ya damu ya mbuzi na ya ndama, lakini aliingia Patakatifu pa Patakatifu mara moja tu kwa damu yake mwenyewe, akiisha kupata ukombozi wa milele. Damu ya mbuzi na ya mafahali na majivu ya mitamba vilivyonyunyiziwa wale waliokuwa najisi kwa taratibu za kiibada viliiwatakasa hata kuwaondolea uchafu wa nje. Basi si zaidi sana damu ya Kristo, ambaye kwa Roho wa milele alijitoa nafsi Yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na waa kutusafisha dhamiri zetu, kutokana na matendo yaletayo mauti, ili tupate kumtumikia Mungu aliye hai!” (Waebrania 9:12-14).

Hakuna lile linalomfurahisha Mungu kama watoto wake wanao kuja kwake na Ujuba mkuu, bila uoga! Anataka tuje tukisema, “Nina Haki ya kuwa hapa! Na hata kama moyo wangu unanihukumu, Mungu ni Mkuu kuliko moyo wangu! (soma 1 Johana 3:20). Mkoma huyu alipomsongelea Yesu mara ya pili, Maandiko yanasema, Yesu “alimfanya Mkamilifu”. “Yesu akamwambia, “Inuka na uende zako, imani yako imekuponya.” Wakati huu Yesu alimbariki na jambo kuu kuliko tu Utakaso, alimbariki na Ukamilifu wa Akili, Mwili, Nafsi na Roho. Na hili ndilo Mungu anawapatia wote wamsongeleao siku ya Leo, Ukamilifu! Napenda kufikiri kwamba Mkoma huyu aliyefanywa kamili alirudi kijini na kuungana tena na wale wengine Tisa. Jameni ni mazungumzo ya ajabu kweli walikuwa nayo! Wale Tisa labda walianza kunena shida zile walizokumbana nazo waliporudi. Bibi zao walikuwa wamekwisha olewa na watu wengine, watoto waliwaepuka kwa aibu, marafiki wakitambo walijifanya wageni kwao, kujiendekeza kulikuwa na Uzito usiowezekana. Wakamgeukia yule Mkoma Msalia, “ilikuwa vipi upande wako?” unamkumbuka yule Mgalilea aliyetuponya? Je unajua habari zake? Na kwanini unakaa mwenye Furaha? Akatabasamu na kusema, “Nilikuwa naye haswa jana! Mimi namfuata yeye – nimekuwa mwanafunzi wake na yeye amekuwa Mwalimu wangu. Namuniamini, sijakuwa na shida ya kujiendekeza! Hainikeri moyo kwamba familia yangu ilinikana, au kwamba rafiki zangu walinikwepa, Yesu alinipokea! Ndugu zanguni hebu niwaambiye – mimi natembea na Mungu! Ananiongelesha na Ananifunza. Nimekuwa mtengeneza Hema sasa – lakini zawadi yangu kuu ni kumsifu Bwana wangu!" labda aliwaalika wale Tisa wajiunge naye kwenda kwa Yesu. Lakini labda wangekataa hoja yake: “pole – tunasoma sheria mara tatu usiku kwa wiki. Tuko na hoja kali tunajadili sasa kuhusu lini Mwokozi wetu atakuja!” labda walifikiri wanamtafuta Mwokozi – lakini walikuwa washamkosa tayari! Basi huyu Mkoma Msalia alirudi kwa Yesu akiimba, “Kuna nyimbo moyoni mwangu hata Malaika hawawezi kuimba – Nimekombolewa, Nimekombolewa!” Anaishi kwa Ukombozi – amefanywa kamili – Huru kabisa!

Mpendwa mtakatifu, mimi na wewe tumebarkiwe na lile kuu kushinda lile alilokuwa nalo huyu Mkoma Msalia. Hatuna tu mlango wazi, lakini Baba mpendwa atuambiaye, “Njoo – Umetakaswa. Amini – Chukua azma kwa Imani. Njoo ukutane na Yesu!” Hallelujah!

---
(Maandiko yamenakiliwa kutoka kwa IBS-STL Global translation http://www.ibs.org/bibles/swahili/index.php)