Wakati Wa Kilio na Wakati wa Vita

Nisomapo Agano la Kale, Imani yangu hupata nguvu na ule mfano wa Daudi. Jambo baya lilikuwa limemfanyikia mtu huyu, mpaka maisha yake yalikuwa yametishwa na wale waliokuwa wandani wake. Ninajengwa Imani na vile Daudi alivyo tafuta neno kutoka kwa Mungu wakati huu wa shida kuu. Ilikuwa hivi: Daudi pamoja na majeshi yake 600 walikuwa wanamtoroka Mfalme Sauli aliyakuwa akitaka kuwaua. Walifika mahali paitwapo Siklagi wakapiga kambi pamoja na familia zao. Kisha wakaenda vitani mabibi na watoto wakiwa wamebaki hapo kambini. Baada ya vita, Daudi na majeshi yake wakaanza safari ya siku tatu kurudi kambini. Kumbe wakati huo, kambi yao ilikuwa imetekwa nyara na kuporwa na Waamaleki. Adui huyu Mbaya aliteka nyara familia za Daudi na majeshi yake na kuchoma hema na kambi yote! Jaribu kutafakari tukio hilo pale Daudi na majeshi yake waliporudi: “Daudi na watu wake walipofika Siklagi, wakakuta mji umeangamizwa kwa moto na wake zao pamoja na wana wao na binti zaowamechukuliwa mateka” (Samueli wa Kwanza 30:3).

Watu hao walipigwa na butwaa walipogundua hayo. Ilikuwa ni mgutuka wakutisha walishindwa kustahimili. Nawaona wakizungukazunguka bila mpango wakilia kwa uchungu. “lingefanyika vipi hili? kwanini Mungu aliwachilia lifanyike?” “Hivyo Daudi na watu wake wakapiga yowe mpaka wakaishiwa na nguvu za kulia.” (Samueli wa Kwanza 30:4). Tukio hili kutoka kwa maisha ya Daudi linatuonesha kuwa kuna wakati wa kulia panapotokea jambo la huzuni. Maandiko yanawataja majeshi ya Daudi kama “Mashujaa”, ikimaanisha wanavita waliopata sugu wasioweza kulia. Lakini tukio hili liliwafanya Mashujaa kulia kwelikweli. Walakini, halikuwa tukio dogo. Si kwamba walipoteza nyumba tu au mimea shambani ililowafanya Mashujaa wa Daudi kulia; kama ingelikuwa hayo, wangepona kwa haraka. Lakini, ilikuwa ni hatari iliyokuwa inawakumba bibi na watoto wapendwa iliyowadunga Nafsi zao. Yaliyofuata yangeishia vibaya kwa Daudi: “Daudi alihuzunika sana kwa sababu watu walikuwa wakisemezana juu ya kumpiga kwa mawe, kila mmoja alikuwa na uchungu rohoni” (Samueli wa Kwanza 30:6).

Tunayoyashuhudia duniani leo yamenakiliwa kwa maandiko: “Kwa sababu BWANA anayo siku ya kulipiza kisasi,mwaka wa malipo, siku ya kushindania shauri la Sayuni.” (Isaya 34:8).

Naamini kupitia misukosuko na balaa zilizoikumba ulimwengu, Mungu ana hukumu tamaa, wivu na majivuno. Ninahakika Hawezi tena kukubali uchafu wa ngono kuharibu Nafsi za kizazi chote. Na ninaamani kwamba ndoa ya ushoga imekuwa kiini cha hikumu hii ya Mungu. Nyakati anazonakili Isaya zilikuwa na kilio, majonzi na uwoga. Walakini, Mungu alimpa Isaya Neno la kujenga moyo akisema, “Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti aliyolegea, waambieni wale wenye mioyo ya hofu, “iweni hodari, usiogope, tazama, Mungu wenu takuja, pamoja na malipo ya Mungu, atakuja na kuwaokoa ninyi.’’ Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa na masikio ya viziwi yatazibuliwa.” (Isaya 35: 3 – 5). Mungu alikuwa anasema kwa hakika: “wainueni moyo waliochoka. Wajengeni wale waliodhoofika kati yenu. Watieni moyo walio na uoga and masononeko. Waambieni, hamna chanzo cha kuwa na uoga. Haya yote yameletwa na Mungu, na kupitia haya, atawakuza watu wake. Anafanya yote haya kuwaokoa ninyi. Wapendwa. Ata wale watakatifu mno kati yetu huingiwa na uoga moyoni pale mikosi inapokuja. Wakati kama huwo, Si dhambi kuwa na uoga kiasi. Kwa kweli, Mungu alipo mpa Isaya neno hili, alikuwa akihakikisha kuwa, wale mabo walikuwa wamepigwa butwa na uoga kwa sababu ya tendeko la ajabu wasiweze kumalizwa na tendeko hilo. Alitaka kila moyo uliokuwa na majonzi usikie: „Usiogope! Kuwa Jasiri, kwa kuwa Mungu ni Mwokozi kwa watu wake.

Baada Ya Wakati Wa Kilio, Huja Wakati Wa Vita

Wakati hufika ambapo kilio chote mpaka kiishe. Wakati huo watu wa Mungu huinuka kutoka kilioni, kutoka kwa masononeko, kutoka kwa upungufu wa aina zote na kuchukua fursa vitani! Katika Agano Jipya, Waebrania anaitikia maneno ya Isaya: “Kwa hiyo itieni nguvu mikono yenu iliyo dhaifu na magoti yenu yaliyolegea. Sawazisheni mapito ya miguu yenu, ili kitu kilicho kiwete kisidhoofishwe bali kiponywe.” (Waebrania 12:12–13). Maanake, “usibaki chini, simama upiganiye Imani yako!” tumikia Imani yako ndani ya Bwana. Usikubali magoti yatikiswe, bali endelea kutimua mbio, ukitegwa na uoga na uanguka, Imani yako inaweza kupoeshwa”. Tafakari tabia ya Mashujaa wa Daudi baada ya tukio lile la kusikitisha. Baada ya kulia majeshi hawa walichukizwa na kuingiwa na hasira. Wakaanza kumlaumu Daudi, walikuwa wamepotoka, wenye chuki kutokana na shida ile, wakaanza kuokota mawe ili wamuuwe Daudi. Kwa maoni yangu, hili ndilo watendao wengi wakati huu wa Janga hili la Uchumi. Wamepofushwa na hasira yao, wanageuka kushoto na kulia wakiuliza, “nani chanzo la janga hili? Watupe wote jelani!”. Ninahimiza wafuasi wa Yesu: sahau vile tulifika hapa. Sahau kabisa kuhusu nani mwenye lawama. La muhimu zaidi, sahau kabisa kusema laiti ingelikuwa: “laiti ingelikuwa kwamba ningefanya hivi ama vile, pesa zangu zingelikuwa salama”. Ukikwamilia mawazo hayo, uoga wako utageuka na kuwa chuki na hasira au roho nyingine chafu ya kuzimu. Hapana! Mungu anataka kugeuza njia, Neno linatueleza, “sasa ndio wakati wakupigania Imani yako!”. Tazamia jawabu la Daudi: alijitia moyo. “Daudi alihuzunika sana kwa sababu watu walikuwa wakisemezana juu ya kumpiga kwa mawe, kila mmoja alikuwa na uchungu rohoni kwa sababu ya wanawe na binti zake. Lakini Daudi akajitia nguvu katika BWANA, Mungu wake. (Samueli wa Kwanza 30:6). Badala ya kuingi uoga, Daudi aliamua kupigana na uoga wake. Naamini alifanya hivi baada ya kukumbuka Uaminifu wa Mungu mara nyingi alipomkomboa kutoka kwa mambo ya kutisha katika maisha yake. Utotoni mwake, Daudi aliua kaka dubu, aliuwa simba na akammaliza jitu Goliathi. Sasa alitafakari vita hivi na nyingine alizoshinda. Kila Ushindi uliletwa tu na Imani yake isiyo tingisika. Daudi alisema: “Nahitaji Neno kutoka kwa Bwana Mungu”. Alijua hakuna mwengine anayeweza kumtia moyo – sio Kuhani wake, Abiatha hata Makapteni wa jeshi lake, hapakuwa na Mshauri kamwe. Ilimlazimu Daudi apate neno kwa yule mmoja aliyemkomboa kutoka kwa majanga yote aliyowahi kupitia. Wapendwa, hivyo ndivyo inafaa kwangu mimi na wewe pia. Hakuna mtu yeyete duniani awezaye kuinua roho yako unapokufa moyo. Hakuna awezaye kuikuza roho yako unapopitia janga. Inatulazima kila mtu tupate neno la kipekee kutoka kwa Mungu. Kama Daudi, tumeitwa tujutie moyo kwa kukumbuka yale makuu Mungu ametenda maishani mwetu. Na lazima tukumbuke nyakati zile Mungu amekuwa wa msaada toka enzi za jadi.

Kuinuana Moyo Kunaweza Tu Kutufikisha Umbali Kiasi.

Kama maubiri usikiayo kutoka kwa Mchungaji wako yana upako, basi yataweka maisha ndani yako. Mauburi katika Neno la Mungu hutia moyo watoto wa Mungu. Sawa tu na vile kuomba na kuabudu kwa pamoja huinua nyoyo zetu kwa mda. Walakini, haraka mno tunashushwa moyo wakati ibada ya juma pili inapokwisha. Jumatatu na jumanne hupita na habari katika runinga zinaaza kuchafuka na wengi tunarudi kwa uoga na kuangaika. Nyakati za kawaida, naweza kupokea ushauri kutoka kwa Mke wangu iliyeokoka, Gwen. Yeye huwa karibu kunipa Neno zuri wakati ninapolihitaji. Namuona vile daudi alivyomuona Abigaili, “Ndipo Daudi akapokea kutoka mkononi mwake kile alichokuwa amemletea naye akasema, “Nenda nyumbani kwako kwa amani, nimesikia maneno yako na kukujalia ombi lako.” (Samueli wa Kwanza 25:35). Lakini mambo yaweza kuwa magumu wakati wa janga. Wakati Imani yetu inapigwa vita – wakati maisha yetu yanapotishwa – mashauri ya mke au mume, wachungaji na marafiki wenye hekima yaweza tu kutufikisha umbali kiasi. Nyakati hizi ni nyakati za shida mno, ukweli ni kwamba, ni Neno la kibinafsi kako kutoka kwa Mungu ndilo liwezalo kutupitisha tukiwa na matumaini ya kudumu. Mungu amekuwa imara na muaminifu kwa kunena Neno kwa watu wake tokea enzi za jadi. Katika Agano la Kale, tunasoma mara nyingi: “Neno la Mungu Likaja...” Maandiko yanasema kuhusu Abrahamu: “Baada ya jambo hili, neno la BWANA likamjia Abramu..:” (Mwanzo 15:1). Tunasoma kumuhusu Yoshua: “Lakini Israeli wakajichukulia mifugo na nyara za mji huu, kama vile BWANA alivyokuwa amemwagiza Yoshua.” (Yoshua 8:27). Na vivyo hivyo ilikuwa na Daudi na manabii wa Mungu. Tunasoma maandakio, “Neno La Mungu Likamjia...” na kwa watu wa Mungu leo, tuko naye Roho Mtakatifu awezaye kunena neno kutoka Mbinguni kati yetu. Kupitia Roho Mtakatifu, faraja, uponyaji na Neno la kutuelekeza liko kwa wale wanaomuamini.

Tafakari wale majeshi 600 waliomfuata Daudi. Walisikia Maneno yale Mungu alimpa kiongozi wao. Lakini Maneno hayo yangetakiwa kwanza yawe hai ndani yao. Ilalazimu iwe kwamba Mungu aongee ndani ya roho zao kibinafsi. Ndio wangeliweza kupata nguvu za kupigana vita. Ndiposa naamini kwa wakati huu, changamoto kwa muamini yeyote yule, ni kukaa katika neno la bwana mpaka Roho Mtakatifu alifanye neno lichangamke na kutoka kwa karatasi za Bibilia mpaka kwa muumuni binafsi. Tutajua linapotendeka kwa sababu tutasikia sauti ya Roho Mtakaitfu iliyo tulivu ikinena ndani “Ahadi hii ni yako. Ni neno la Mungu kwako, lililoletwa likupitisha katika nyakati za shida.”

Daudi Alijitia Moyo, Akarejesha Ujasiri Na Papo Hapo Akatenda Kulingana Na Imani Yake.

Daudi aliporejesha ujasiri wake, aliitisha Kisibau. Hii ilikuwa nguo maalum inayovaliwa kifuani mwa Kuhani iliyokuwa na mawe mawili. Wakati mwingi, Mungu alinena kupitia Kisibau. Na Daudi aliamua kupata Neno La Bwana la kumuelekeza mbele. “Kisha Daudi akamwambia kuhani Abiathari, mwana wa Ahimeleki, “Niletee kile kisibau”. Abiathari akamletea, naye Daudi alimwuliza BWANA, “Je, nifuatie kundi hili la wavamizi? Je, nitawapata?” (Samueli wa Kwanza 30:7–8). Tafakari mambo Daudi alifanya hapa, baada ya kulia, alirejesha nguvu, kisha akapiga magoti mara moja. Mungu akampa Neno la kumuelekeza, Mungu alimjibu ”Wafuatie. Hakika utawapata na utafanikiwa kuwaokoa” (Samueli wa Kwanza 30:8). Neno la Mungu kwa Daudi lilikuwa “enenda, utapata ushindi”. Kwa njia nyingine: “Kaa ngumu vitani, usife moyo!” Tunasoma yafuatayo katika Maandiko, “Daudi pamoja na watu wake 600 wakafika kwenye Bonde la Besori,” (30:9). Daudi mara moja alitenda kulingana na Neno la Mungu, lakini mimi nashangaa Daudi alijuwaje mahala pa kuenda? Ni njia gani angelifuata ili apate kurejesha yote yaliyoporwa? Ninaamini kulikua na Sauti nyuma ya Daudi ikimnenea, “hii ndio njia, pita hapa” wapendwa, vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwetu wakati huu. Kanisa nyingi huimba nyimbo hii inayojenga moyo sana, “He will make a way,- Mungu atajenga njia” na kwa kweli Bwana wetu atenda vivyo hivyo haswa. Jameni, Mungu alikuwa na mpangilio maalum hata kabla ya janga kutokea. Na mpangilio huwo unaendelea vilevile alivyoipanga hata katika majanga haya tunayo kumbana nayo. Ninahakika Neno alilowaza Daudi kila mara lilikuwa, “Utafanikiwa Kuwaokoa wote!” Daudi alijuwa vizuri kabisa hata pata tena nyumba yake iliyokuwa pale Sikilagi. Majeshi wake nao pia hawange rejesha nyumba zao, shamba na mali. Hayo yalikuwa yamepotea yote. Hapana, “yote” watakayofanikiwa kuokoa ilikuwa ni usalama na uzima wa jamii zao. Unaona sasa ufananisho na nyakati zetu? Watu hawa hawakuwa warejeshewe maisha yao ya kale. Hawakuwa warudi kwa maisha ya utulivu, maisha hayo ya kitambo yalikuwa yamepitwa na wakati. Hayo sio yaliokuwa yakiwasumbuwa Daudi na majeshi yake 600, walikuwa wakijali tu jamii zao –lililomuhimu – tutakuwa na usalama. Labda iliwabidi kukaa kwa Hema na wake na watoto wao baada ya hayo yote. Lakini Mungu aliwahakikishia kwamba watakuwa salama.

Mungu Hakumueleza Daudi Vile Atamkomboa Akiwa Pamoja Na Jamii Yake.

Wapendwa, Mungu hata tueleza vile atawashugulikia wapendwa wetu, hata tuonesha vile atatuweka salama katika nyakati za janga. Njia zake ni zaa ajabu mno, huwezi ata kutafakari, hatutaweza kamwe kuyafafanuwa maisha yetu yote hapa duniani. Kwa Daudi, ukombozi ulitoka mahala ambapo hangeweza kudhania: kijana Mmisri aliyekuwa akielekea kufa. Mtumwa huyu kijana alikuwa karibu kufa Daudi alipompata jangani na kumpa maji na chakula. Daudi alipomuuliza, “wewe ni nani?” natumai Mungu alimnong’onezea Daudi, “Daudi, huyu ndiye ukombozi wako!” jameni, lakustaajabisha vipi, njia za kumiujiza za Mungu! kijana Mmisri aliyekuwa kifoni ndiye alikuwa awaelekeze Daudi na majeshi yake kambini mwa Adui. Kwa ufupi, Mungu alimtumia kijana asiyekuwa hata na Jina kuongoza watu wake kuokowa yote.

Nikifunga somo hili, nitawapeleka tena kwa Isaya 35.4: “waambieni wale wenye mioyo ya hofu, “iweni hodari, usiogope, tazama, Mungu wenu atakuja, pamoja na malipo ya Mungu, atakuja na kuwaokoa ninyi.’’ Wakati dunia inapokumbwa na malipizo – wakati mambo yote yanaenda mrama – Mungu yuko katika juhudi ya kutuokoa. Anatumia hata misukosuko ya janga za ulimwengu kuleta wokovu. Yeye ni Muaminifu na ni Mwokozi, atawakuza watu wake, kupitia majanga yote.

Maandiko yamenakiliwa kutoka kwa IBS-STL Global translation http://www.ibs.org/bibles/swahili/index.php)