VYOMBO VYA UTUKUFU WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu hakukusahau wewe! Anajua hasa mahali ulipo, unachofanya nini hivi sasa, na anaangalia kila hatua kwenye njia yako. Mara nyingi wakati wa mgogoro, Wakristo husahau kwamba Mungu anao katika kigiganja cha mkono wake. Badala yake, kama wana wa Israeli, walivyoogopa kuwa wataangamizwa na adui. Mungu lazima avutie kuelewa kwa nini watoto wake hawakumwamini wakati wanapokuwa chini na wanahitaji. "Je! Hawajui kwamba mimi nimewandika kwenye kiganja cha mikono Yangu? Sikuweza tena kuwasahau katika saa yao ya mahitaji kuliko mama anaweza kumsahau mtoto wake mchanga" (angalia Isaya 49:15-16).

Mara kwa mara Mungu alikuja kwa Israeli akiwaombea kwa uwaminfu wao na kuamini kwao wakati wa magogoro. "Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mutaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali" (Isaya 30:15).

Inaonekana hata Agano Jipya linaonyesha hasira ya Mungu kwa kutokuamini: "Omba kwa imani, pasipo shaka yo yote, kwa maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku nako. Maana mtu huyo asidhani kwamba atapokea kitu chochote kutoka kwa Bwana; yeye ni mwanadamu mwenye nia mbili, hawezi kudumu kwa njia zake zote" (Yakobo 1:6-8).

Je! Umewahi kuhisi kwamba Mungu amekukana na kukuacha ujionee mambo mwenyewe? Badala ya kuwasilisha kwa Bwana kwa ujasiri wa utulivu na kupumzika katika ahadi zake, huenda umejaribu kupata ufumbuzi wako mwenyewe na mambo ameptelea mbele ya uso wako.

Uwe na hakika kwamba Mungu anataka kukutana na mahitaji yako yote, lakini zaidi ya yote, anataka ushirika upya na wewe. Rudi kwenye chumba cha siri cha maombi na imani rahisi, kama mtoto. Usifanye kazi sana juu ya Mungu ili umsahau yeye anaejaribu kufanya kazi kwako, kwa akakufanya kuwa chombo cha utukufu.