UZAIFU UNAOSHANGAZA KWA MUNGU

Gary Wilkerson

Kwa kuandikia kanisa la Korintho, Mtume Paulo anachangia mawazo yake kwamba ujasiri wao kwa Mungu unapungua. Baadhi ya tamaa yao ni kuhama, kusonga-katikati, na lengo lao si wazi, kwa hiyo anawatumia barua ya kurekebishwa kwa nguvu.

"Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri! ... Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye akili katika Kristo. Sisi tu dhaifu, lakini ninyi mna nguvu; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima. Hata sasa hii ya sasa, tuna njaa na kiu, tuuchi, twa pigwa ngumi, tena hatuna makao; kisha twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu yenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twastahimili; tukisingiziwa twasihi; tumefanywa kama takatak za dunia, na tama ya vitu vyote hata sasa. Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuaonya kama watoto niwapendao" (1 Wakorintho 4:8, 10-14).

Wasomi wanatuambia kwamba kanisa la Korintho labda lilikuwa tajiri zaidi kuliko makanisa yote ya Agano Jipya. Eneo lao liliwapa fursa nyingi za utajiri mkubwa kutoka sekta ya meli. Paulo alikuwa akiwaelezea kwamba walionekana kuwa na vitu vingi kama jamii iliyowazunguka; wakati walipokuwa na vitu vyote vikubwa vyenye kuwaendea, kunakitu kilikuwa kinakosa. Hata kwa mafanikio yao ya nje, ndani kulikuwa na kitu kibaya.

Nini kilichoendelea katika kanisa hili? Paulo hakuwahi anawaonya kwa kuwa wanafanikiwa au kuashiria kuwa masikini kwa namna fulani ilikuwa bora. Hapana! Alikuwa akionyesha kuwa lengo lao lilikuwa si sawa. Walikuwa wakijaribu kutimiza tamaa zao za mioyo, na mambo ya ulimwengu huu badala ya kumtafuta Mungu kwanza. Kwa maneno mengine, walikuwa wanatafuta upendo katika maeneo yote mabaya. Na kwa sababu hii, maisha yao hayakuwa na matokeo kwa ufalme wake. Vivyo hivyo, leo, tunapaswa kuwa makini ili tusitosheke na mambo ambayo yanatuondoa kwenye maono wazi ya Yesu!