UTUKUFU WA MUNGU UNA FUNULIWA KATIKA MISIMU MIGUMU

Gary Wilkerson

Neema ya Mungu inakufuata! Hii siyo tu maneno ya kukuhimiza wewe, ni kweli kulingana na kifungu baada ya kifungu cha Maandiko. Hata hivyo wachache sana katika kanisa wanaishi kama hii ni kweli.

Unaweza kuwa na migogoro ya ndoa na kujiuliza kama mvutano na mwenzi wako utazunguka zunguka milele. Au huenda unakabiliwa na unyogovu na kushangaa kama utaweza kuinua ili uweze kuhisi kibali cha Mungu tena. Labda una mtoto mpotevu na unajiuliza ikiwa atarudi tena kwa imani. Au labda una ndugu ambaye ni anajihusisha na mambo mabaya, na kushangaa kama yeye atoka utumwani wake baada ya miaka mingi ya kua kwenye tabia yake.

Ninaweza kukuhakikishia kwamba hakuna Mkristo aliyewahi kujichola mwenyewe akiwa katika misimu kama hii. Hakuna mtu aliyewahi kufikiri matatizo ya kudumu yanayodhuru faraja wanayosikia kutoka kwa Mungu. Lakini Petro anatuambia kama hatupaswi kufikiria kuwa majaribu kama haya ni ya kawaida: "Wapendwa musione kuwa ni ajabu ule musiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe." (1 Petro 4:12-13).

Ikiwa uko katikati ya msimu mbaya wa maisha, nina neno la uhakika kwako: Kumbatia! Bwana hajamaliza pamoja na wewe. Unaweza kufikiria wewe peke yako katika shida yako, lakini kila kando Mungu amekuwa akihifadhi baraka kwa ajili yako ambazo haujawahi kuota. Kama Petro anasema, utukufu wake utafunuliwa kupitia jaribio lako.