UTOAJI MKUBWA WA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Mtu mmoja aliniambia mara moja, "Baada ya kutoa asilimia kumi ya mapato yangu kwa Mungu, mimi napendezwa na kitu chochote kinabakia. Na ninatarajia kubarikiwa na Mungu kama alivyoahidi - kwa sababu nilitoa fungo la kumi."

Uzoefu wangu umesisitiza kwamba kama mtu ananungunika kwa kutoa kwake, atakuwa pia ananungunika wakati wake, nguvu zake na kazi yake kwa Bwana. Lakini nataka kukuambia, ikiwa unadanganya na Mungu, atakudanganya na wewe. Kwa hiyo, nina maanisha kwamba uko unakata wewe mwenyewe Baraka kutoka kwa Mungu kupitia matendo yako na mtazamo wako.

Tabia yetu inapaswa kuwa, "Ni kiasi gani cha nafsi yangu ninaweza kumpa Bwana wangu?" Heri yetu inapaswa kuwa katika kiasi gani tunaweza kutoa, si kwa kiasi gani tunaweza kujiwekea.

Tunasoma katika Neno, "Bali kwao wakemeao furaha itakuwa; na Baraka yafanikiwa itawajilia" (Mithali1:24:25). Ukweli ni kwamba, nguvu zaidi na nguvu ambazo unatumia kwa ajili ya Mungu, zaidi atakumwangia tena ndani yako.

Mtume Paulo alihisi kila hisia na majaribio tunayopata, lakini kwa njia yote yeye alikuwa na ufunuo wa rasilimali zilizopatikana kwake. Alipokuwa amezidiwa, imani yake imeshikilia yote ambayo aliohitaji ili kumleta kwa kushinda! Alichota juu ya rasilimali za Baba yake wa mbinguni na akaongezeka mara kwa mara na imani mpya na nguvu mpya za kuendelea.

Katika kujitolea kwa moyo wote kwa kazi ya Mungu, unajiweka katika nafasi ya kubarikiwa. Ikiwa munafikiri juu kuacha, nawahimiza kukaa katika vita, kwani ni katika joto la mapigano ambayo Mungu anakuja kwako kwa ukarimu, akiwaonyeshea kwa rasilimali zake na nguvu zake. Ni wale tu waliohusika katika vita wanapokea utoaji wake mkubwa!