"USIOGOPE!"

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu ametuamuru tusiwaogope adui zetu. "Usiwaogope" (Kumbukumbu la Torati 7:18). Kwa Israeli, "wao" waliwakilisha uwingi wa mataifa wakipagani, yenye kujihami na silaha zenye nguvu ambayo walikabili katika Nchi ya Ahadi. Kwa sisi leo, "wao" inawakilisha tatizo lolote, shida na matatizo magumu tunayopata katika maisha.

Mungu anasema tusiogope, kwa hiyo hakuna maelezo mengine yanaohitajika. Mungu ni nguvu zote na anajua ngome za shetani tunazokabiliana nazo - kila mtego, magumu na majaribu. Lakini bado anasema, "Usiogope lolote kwa hao!"

Mungu alimwambia Ibrahimu, mtu aliyeishi katika nchi ya ajabu na akizungukwa na wafalme wenye nguvu, asiwe na hofu. Abrahamu hakuwa na ufahamu ambapo angeweza kuishia lakini Mungu aliahidi kuwa ngao yake na tuzo kubwa sana (Mwanzo 15:1). Mungu alikuwa akimwambia Ibrahimu, "Wewe utakabiliwa na shida, lakini nitakukinga kupitia hao yote." Na Ibrahimu akajibu kwa kuamini neno la Mungu kwake: "Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki" (15:6).

Neno hilo hilo lilikuja kwa mwana wa Ibrahimu, Isaka. Pia aliishi katika mazingira ya chuki, akizungukwa na Wafilisti ambao walimchukia na kumtesa. Walitaka aondoke kutoka ardhi yao, na Maandiko yanasema kwamba Wafilisti walijaza  udongo visima ambavyo Ibrahimu alikuwa amechimba na kuviachia Isaka (angalia Mwanzo 26:15). Isaka alijisikia kuingia ndani mgogoro maishani muake yote na lazima awe na wakati huo lazima awe na mawazo, "Mungu, kwa nini umenipandkiza hapa?" Lakini Mungu akasema: "Usiogope, maana mimi ni pamoja nawe. Nitawabariki na kuzidisha uzao wako" (26:24).

Sisi pia ni watoto wa Ibrahimu, na Mungu hufanya ahadi ile ile kwetu aliyofanya kwa Ibrahimu na watoto wake: "Nakama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahim, na warithi sawasawa na ahadi" (Wagalatia 3:29). Baba yetu wa mbinguni anaona kila hatua ya maisha yetu na licha ya shida zetu zote na matatizo, anatuamuru mara kwa mara katika Maandiko, "Usiogope!"