USHIRIKA PAMOJA NA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Upendo wetu wa kidunia hubadilika, wakati mwingine kila siku, huenda kutoka kwa moto na bidii hadi kwenye joto au hata baridi kama hisia zetu zinabadilika. Kama wanafunzi, tunaweza kuwa tayari kufa kwa Yesu siku moja na kisha kuwa tayari kumsiacha na kukimbia ijayo. Tunaweza kumwambia Bwana tunamwamini kuwasilisha mahitaji yetu yote na bado tunakaribisha shaka na hofu wakati hali yetu inabadilika.

Upendo wa Mungu kwetu bado haubadilika. Neno lake linasema, "Mimi ni Bwana, sina kigeugeu" (Malaki 3:6). Na katika Yakobo 1:17: "Kila kutoa kuliko kwema. . . hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka."

Tunapokuwa katika ushirikiano wa kweli pamoja na Baba, sisi sio tu kupokea upendo wake lakini tunarudisha kwake pendo hilo. Huu ni upendo wa kushirikiana: wawili kutoa na kupokea wote upendo. Biblia inatuambia, "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote" (Kumbukumbu la Torati 6:5). Anatuambia pia, "Mwanangu, nipe moyo wako" (Mithali 23:26). Upendo wake kamili unahitaji kurudishina, kurudisha upendo ambao umekamilika, usiogawanyika.

Bwana hutuambia bila yakuwa hakuna uhakika: "Huwezi kupata upendo wangu. Upendo ninayowapa hauwafai." Yohana anaandika, "Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba Yeye alitupenda sisi, akumtuma Mwanawe kuwa mpatanisho wa dhambi zetu " (1 Yohana 4:10). "Tunampenda kwa sababu Yeye alitupenda kwanza" (mstari wa 19).

Mungu alifikia chini ya jangwa la maisha yetu, alituonyesha upotevu kwetu, na kutufanya sisi kuwa masikini katika dhambi zetu. Alitutumia Neno lake ili lituonyesha ukweli, alimtuma Roho wake kutuwezesha kukubali makossa yetu, na kisha akaja mbere yetu mwenyewe. Kwa sababu ya hili, tunapo kumkubali katika maisha yetu na kukaa katika ushirika pamoja naye, tunaweza kutembea katika usalama na utulivu, kamwe hatuwezi kuwa namashaka.