UPUMZIKO MZURI KATIKA BWANA WANGU

David Wilkerson (1931-2011)

"Mbele za uso wako ziko furaha; na katika mkono wako wa kuume mna mema ya milee" (Zaburi 16:11).

Wakristo wanaongezeka zaidi kwa kutopendezwa na jinsi mambo yalivyo duniani na katika kanisa. Watakatifu hawa wanasema, "Mungu ana kitu zaidi kwetu! Anatuita tujue yeye vizuri na tunataka kutembea katika utii kwa wito huo." Wao wanaanza kufunga na kuomba katika jitihada zao kwa kina kirefu kiroho.

Wakati Bwana anataka kukugusa kusikokawaida, atagewuza kiota chako. Ukosefu usio na maana wa Mungu utakujia na utakuwa na wasiwasi katika mengi ya yale uliyokuwa ukifanya katika maisha yako. Mafanikio yako yote yatakuacha uhisi utupu na kutojazwa, na utaona haja ya kina, isiyo na kipimo katika roho yako.

Ishara ya ushujaa huu usiowakawaida ni moyo wenye njaa. Kila saa ya kuamuka moyo wako utamfikia kwake, tena fikiri zake zitakuwa kwenye mawazo yako daima . Mungu anataka utoke kwenye mambo ya ulimwengu huu na kupata ukamilifu wako wote ndani yake.

Je! Nafsi yako ina njaa zaidi ya Roho Mtakatifu katika maisha yako? Je! Unaona wito wake kwa kutembea zaidi na Mungu? Ikiwa ndivyo, maliza vita ndani ya moyo wako kwa kutoa kila kitu kwa Mwalimu. Unaweza kujua amani ya kweli na furaha wakati unaacha kujitahidi kupata mafanikio makubwa au zaidi "vitu" ili kukidhi mahitaji yako mwenyewe. Usitafute kitu kingine ila Yesu mwenyewe, na maisha yako atachukua maana mpya. Wasiwasi itakwenda, tamaa ya kidunia itakufa, na macho yako ya kiroho atafunguliwa kwa ukweli.

Wakati Roho Mtakatifu anakupa ufunuo wa ujuzi, utaona utajiri wa kweli katika Kristo Yesu. Wewe utaamka asubuhi kila siku ukiwa na furaha yenye kufurika, na roho yako itasema, "Nimeona kitu ambacho nafsi yangu imetamani muda mulefu. Pumzika - mapumziko mazuri katika Bwana wangu."