UPENDO WAKE HAUNA MWISHO

David Wilkerson (1931-2011)

Kulingana na Yesu, katika macho ya Baba, Kristo na Kanisa lake ni wamoja. Paulo anaonyesha hii kwa mfano wa mwili wa mwanadamu. Anasema Kristo ndiye kichwa, na sisi ni mwili wake - mfupa wa mfupa wake, mwili wa mwili wake. "[Mungu] akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa ;ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.” (Waefeso 1:22-23). “Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake" (Waefeso 5:30).

Je, hapa unaona uingiliano? Wakati Baba alimpenda Yesu milele na milele, alitupenda milele na mile pia. Kwa hakika, wakati mtu alikuwa wazo tu katika akili ya milele ya Mungu, Bwana alikuwa tayari kwisha kuhesabu sehemu zetu na kupanga ukombozi wetu.

"Kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla yakuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu,watu wasio na hatia mbele zake katika pendo" (Waefeso 1:4).

Mungu alimpenda Mwana ye pamoja na sisi daima. Upendo wake ni wa milele kama yeye anavyosema: "Nimekupenda kwa upendo wa milele" (Yeremia 31:3). “Mungu Baba yetu, alietupenda akutupa faraja ya milele" (2 Wathesalonike 2:16).

Hakuna mtu anayeweza kupata upendo wa Mungu kwa kitu chochote cha kimungu anachofanya. Yesu hakupata upendo wa Baba yake kwa kwenda msalabani, au kwa utii wake, au kwa kumpenda Baba yake. Kama hivyo, Mungu hakuanza kukupenda siku ile uliyotubu na kumpokea Kristo. Hakukupenda ghafla wakati ulipoanza kutii Neno lake na kutembea katika Roho. Ulikuwa tayari umependwa tangu milele.

Ni mudagani Mungu alianza ku kupenda? Amekupenda tangu alipoishi, kwa sababu Mungu ni upendo. Ni asili yake sana. Alikupenda wewe kama mwenye dhambi. Alikupenda wakati ulikua tumboni. Alikupenda kabla ya ulimwengu kuanza. Hapo hakukuwepo mwanzo wa upendo wa Mungu kwako, na hakuna mwisho kwa hilo.