UJUMBE PEKE YAKE HAUTOSHI

Jim Cymbala

Wanafunzi walikuwa na nia ya kuanza kuhubiri lakini Yesu aliwaagiza "Lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu" (Luka 24:29). Yesu alijua vizuri zaidi kuliko wanafunzi, kwamba vifaa vinavyohitajika kwa kazi ilikuwa zaidi ya akili nzuri, talanta ya binadamu, na hata moyo wa kweli. Kwa hiyo walitii agizo la Yesu na walisubiri chumba cha juu, wakiomba na kuimba, pamoja na kumsifu Mungu.

"Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafla toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyo wajalia kutamka” (Matendo 2: 1-4).

Roho alimwagiwa kama Yesu alivyoahidi. Nini nabii Yoeli alitabiri kilichotokea. "Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu nab inti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto” (Matendo 2:17). Hii ilimaanisha kwamba aina mpya ya uwezo ilipatikana. "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu" (Matendo 1:8). Nguvu hii ya ajabu kutoka mbinguni ilitakiwa duniani ili kujenga ufalme wa Kristo.

Je, wanafunzi hao walikuwa waumini wa kweli wa Yesu waliomngojea Yerusalemu? Ndiyo. Je, Walikuwa na mafundisho sahihi? Ndiyo. Je, wangeweza kwenda na kuhubiri bila Roho Mtakatifu? Nina hakika walitaka hilo, lakini Yesu alijua hawakua tayari. Alijua uwezo wa adui watakaokabiliyana, kukata tamaa, na upinzani. Ikiwa nguvu ya Roho Mtakatifu ilitakiwa basi, Je, kuna kitu chochote kilibadilika hadi siku ya leo? Je, patakuwa kitu kingine isipokuwa nguvu ya Roho kufanya kazi kupitia kwetu na kubomowa kuta za kutokuamini na kuvunja nguvu za tabia ya dhambi tunapoongea kuhusu injili?

Jim Cymbala alianza na Brooklyn Tabernacle akiwa na wanachama wasio zidi ishirini katika jengo la chini katika sehemu ngumu ya mji huo. Mzaliwa wa Brooklyn, yeye ni rafiki wa muda mrefu wa David na Gary Wilkerson.