UJASILI NA UHAKIKA

Gary Wilkerson

"Ya kwamba yeye alianza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo. Vile vile kama ilivyo wajibu wangu kufikiri haya juu yenu nyote; kwa sababu nyinyi mmo moyoni mwangu" (Wafilipi 1:6-7).

Hapa unaweza kuona upendo Paulo alikua nao kwa Wafilipi. Na kwa sababu ya upendo huu mkubwa, yeye aliwumizwa pamoja nao kwa sababu ya hali ngumu walikua wanapitiya.

Miaka michache iliyopita marafiki wengine wapendwa wetu wote walipoteza kazi zao na walipaswa kuingia katika nyumba ndogo na watoto wao.

Bila shaka, niliwumizwa kwa ajili yawo na kama baba aliye na mtoto, nilitaka kitu kizuri kwao. Lakini unafanya nini unapoumizwa kwa ajili yawengine? Katika hali hii, sala yangu kwa marafiki hao ilienda kama hiki: "Bwana, kwa nini? Nini tatizo? Bwana, huwezi kuwasaidia? Kuwapa kila kazi." Nakubali kwamba nilikuwa na wasiwasi juu ya hali yao.

Tofauti na sala ya Paulo: "Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo, siku zote kila niawaombeapo ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha" (Wafilipi 1:3-4).

Hakukuwa na wasiwasi, hofu, shida, au ukosefu wa ujasiri. Paulo alikuwa anatowa shukrani sana na aliomba kwa furaha kubwa! Je, hiyo inatoka wapi? Hebu tuangalie kile Paulo anatuambia katika mstari wa 6 wakati mwingine.

"Na una uhakika juu ya hili." Uhakika wa nini?

"Kwamba yeye alianza kazi nzuri . . ." Paulo anasema sababu anaweza kuwa na uhakika na sababu anaweza kuwa na furaha ni YEYE . . . Yesu! Anatoa ujasiri na uhakika.

Uaminifu unakuja kwa waumini katika Kristo Yesu wakati wanaweza kusema maneno haya: "Nina uhakika juu ya hili, kwamba YEYE . . ."

Mkazo ni juu ya YEYE. Yeye ndiye aliyefanya jambo hili. Sio daktari. Sio mtalamu wa kifedha. Ni Yesu ambaye alianza kazi njema ndani yako na atakuwa mwaminifu kuitimiza!