UAMINIFU KATIKA DHORUBA

David Wilkerson (1931-2011)

Baadhi yenu kusoma ujumbe huu muko katika dhoruba ya maisha yenu.

Wanafunzi wa Yesu walivumilia mawimbi yaliyopigwa kwa bahari wakati Mwalimu wao amelala usingizi. Hatimaye, kama dhoruba iliendelea kunyemelea mashua, wakamwomba Yesu, wakimshtaki kuwa hajali juu ya hatima yao. "Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?" (Marko 4:38). Yesu alikemeya dhoruba lakini hakuwa na wasiwasi kwa kukosa imani kwa wanafunzi wake. Aliuliza, "Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?" (4:40).

Hivi sasa unaweza kukabiliwa na dhoruba kali katika maisha: shida za fedha, shida ya ndoa, matatizo ya kazi, maadui wanaokuja kwako kama mawimbi makali. Bahari ya shida huwa ndani yenu, lakini Bwana anaonekana kuwa amelala kwa njia hiyo yote. Niambie, imani yako imepigwa? Je, ni pole pole kwa kila tamaa mpya? Labda unalia kutokan moyoni mwako, "Mungu, hujali wewe? Je! Utaniruhusu niende chini katika dhoruba hii?"

Ni kwa muda kama ule tu ambapo Yesu alinena maneno haya ya kushangaza: "Na Mungu Je! Hatawapatia haki (kulinda) wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye nimuvumilivu kwao? Nawaambia atawapatia haki upesi;walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! ataiona imani duniani?" (Luka 18:7-8).

Kumbuka swali la Yesu hapa: Je, atapata imani katika watu wake kama gisi wanavumilia siku za giza na dhiki? Katika miaka ya hivi karibuni nimejiuliza ikiwa Yesu angeuliza swali hilo leo. Kwa miongo mingi watu walikuja kwenye makanisa. Lakini kile ambacho Yesu anauliza kwa kweli ni, "Je! Imani ya hawa itaweza kutokea wakati dhoruba za kutetemeka zinakuja?" Matatizo yetu yanaweza kuwa mapana sana, na kutetemeka kwa mataifa kunaweza kuja haraka sana, kwamba wengine watapoteza tumaini na kuacha. Nawauliza: Je, Yesu atakupata wewe mwaminifu katika saa yako ya dhoruba?