UAMINIFU BILA MIPAKA

David Wilkerson (1931-2011)

"Nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu wenu" (Kutoka 6:7).

Mungu anatamani wewe umjue! Yeye anataka kukufundisha kutambua sauti yake kuliko wengine wote. Alijifunua na kujidhihirisha kwa watu wake, wana wa Israeli, tena na tena - kwa njia ya ukombozi mkubwa na ishara za miujiza - na bado walikuwa hawajui Mungu wao.

"Kwa miaka arobaini nilihuzunika na kizazi hicho, Nikasema, Hao ni watu ambao waliopotoka mioyoni mwao, na hawakuzijua njia Zangu” (Zaburi 95:10). Mungu alikuwa akisema, "Katika mambo yote haya hamkuniacha mimi kuwa Mungu. Bado mulikuwa munatenda kama wenye hawajui jinsi ninavyofanya kazi!”

Mpendwa, Mungu bado anatafuta watu watakaomruhusu kuwa Mungu wao hadi wanapomjua kweli na kujifunza njia zake. Sisi ni kama Israeli kwa kuwa tumeshuhudia miujiza, uzoefu wa udhihirisho wa uwepo wake na maombi yetu yakajibiwa. Tunamwamini Mungu katika maeneo mengi ya maisha yetu lakini imani yetu daima ina mipaka. Kunawezekana kuwa na eneo moja dogo ambalo unazuia ambapo hauamini kabisa Mungu kama atafanya. Mashaka yako inamzuia Mungu kuwa yote ambayo anataka kuwa katika maisha yako.

Mpendwa msomaji, siwezi kusema ikiwa unamjua Mungu kweli kama Yeye anataka. Roho Mtakatifu tu ndiye anayeweza kufunua jambo hilo. Lakini wacha nishiriki nawe kile ambacho Mungu amenifunulia juu ya jinsi ambavyo nimemzuia yeye kuwa Mungu katika maisha yangu: kwa kutopumzika katika upendo wake kwangu.

Ni wakati wa wewe kupumzika salama katika upendo wa Mungu! Lazima usimame na kusema, "Sitakubali mashtaka ya ibilisi - kwa sababu sitastahili kabisa. Thamani yangu yote inakuja kupitia kwake Yesu! Amenitakasa kwa damu yake."

Unaona, huwezi kumruhusu kuwa Mungu wako isipokuwa tu unamruhusu akupende!

Wakati adui anakuja kama simba angurumaye, usiogope - pumzika tu. Sema, "Mungu ananipenda - Yesu ananipenda. Ninajua na ninaamini upendo wake!" Acha awe Mungu kwako kwa kumuonyesha utapumzika katika upendo wake. Kukubali - na ufurahie. Mungu ni bora kuwa Mungu wako wakati unamruhusu akuoshe kwa upendo wake.