TABIA MBAYA

David Wilkerson (1931-2011)

Mara moja nilihubiri mahubiri kuhusu haja yetu ya kuonyesha upendo kwa wale walio karibu na sisi. Nilizungumzia kuhusu dhambi ya kuwa na hasira kwa urahisi - na Roho Mtakatifu alinihukumu mimi dhambi hiyo katika maisha yangu. Nimejifunza kwamba wakati Roho Mtakatifu akisema, hulipa kusikiliza. Nilihubiri mara moja na kisha, baada ya maombi mengi na kumtafuta Mungu, niliamini kuwa nilikuwa na ushindi juu ya udhaifu huo.

Mimi "nilitembea ndani ya ushindi" kwa muda wa siku nne wakati mazungumzo ya simu na rafiki wa karibu, bila kutarajia kwamba niliwasha moto wa asila na kiburi ndani yangu. Nilikuwa na wasiwasi sana kwamba sikuweza kukaa makini juu ya Bwana na nimeanza kumshtaki Shetani kwa kutumia rafiki yangu kunidhuru. "Mungu, shetani alikuwa akimtumia kunikokotea kutenda dhambi."

Mungu hakuruhusu mtazamo kuwa mbali yangu katika mazingila hao na akazungumza nami katika sauti, ndogo, "Daudi, unajishughulisha na mwili wako. Wewe unaruhusu maumivu yako ya zamani na tamaa kukudhibiti - na unachofanya ni hatari."

Nikaona kwamba msisimko wangu haukuwa matokeo ya moja kwa moja ya mazungumzo yaliyoumiza, ni kwa sababu nilikuwa nimeshuka tena katika tabia ya kale niliyofikiri kushinda – na kuruhusu mambo kuingizwa ndani yangu (Angalia Waefeso 4:26-27). Wakati utambuzi huu ulinipiga, nililia mbele ya Bwana, "Je, siwezi kujifunza? Wewe umenipa ujumbe huu na niliwahubiria kwa umati mkubwa wa watu, lakini sikuweza kamwe kutembea katika eneo hilo la ushindi mimi mwenyewe."

Nilihisi kama mchezaji aliyeanguka katika mbio na nikalia, "Bwana, nataka sana kushinda tuzo la kufanana na mfano wako (Angalia Warumi 8:29). Baada ya miaka yote ya kutembea pamoja nawe, bado sija kuja karibu na alama. O, Mungu, nataka kuwa kama Yesu!"

Tii sauti ya uwaminifu ya Roho Mtakatifu na utafute uso wa Bwana. Utashangaa jinsi atakavyokuwezesha kurejea haraka kwa ushindi.