SUBIRA YA KUFUATA UKWELI

Gary Wilkerson

Mtume Petro anatuambia, "Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo. Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, amabayo sasa yamehubiriwa Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni" (1 Petro 1:10-12).

Tunapaswa kutambua kwamba manabii hawa walijua yale waliyoitwa kufanya - kutabiri na kusema Neno la Mungu. Walizungumza neno la nguvu kwa sababu walikuwa na uhakika yay ale  yaliyo ndani ya mioyo yao na walitaka kuwa na uhakika wakuelewa mafanikio ya yale kabla ya kuyawaambia watu. Wao "waliyafanyia uchukuzi na kuyachunguza kwa uangalifu," kutafuta ukweli kwa subira. Ikiwa hatujali, tunaweza kukabiliana na Neno la Mungu kwa kawaida na kusoma tu sehemu tunayopenda. Lakini ikiwa tutafanya hivyo, tutapoteza ukweli ambao tunatarajia sisi kushikilia. Kwa hiyo, ni muhimu tufanye uchunguzi wa neno kwa bidii.

Je, kuna eneo katika maisha yako ambayo haiwezi kudhibitiwa? Inaweza kuwa tatizo linatokana na dhambi au mahusiano. Au inawezakana kwa sababu hutaki kufungua moyo wako kwa utimilifu wa Neno la Mungu na kuomba Roho Mtakatifu kuweka Neno kwa moyo wako.

Ninaamini kweli kwamba Mungu alitupa vitu vyote katika Maandiko kwa ajili ya manufaa yetu, faida yetu, mafundisho yetu, kutukosowa na kuturekebisha. Anataka tuwe watu wazima wenye kuwa na ukamilifu ndani yake. Lakini ikiwa hatuwezi kujitolea wenyewe kwa ukweli wote, hatutaweza kufaidika nawo. Na kama hatuisikilizi Roho Mtakatifu tunapojifunza Neno, tunaweza kuamini mambo ambayo hayapo kwa muda huo.

Ni muhimu sana kuwa sio tu kujua Neno la Mungu, lakini kwamba unajua Mungu wa Neno.