SIPENDI KUSIKIA HILO

David Wilkerson (1931-2011)

Je! Umewahi kujiuliza kwa nini wanafunzi walikuwa hawajui njia za Kristo na madhumuni ya milele ya Mungu? Kwa nini, baada ya miaka mitatu ya kukaa chini ya mahubiri yanayobarikiwa ya Mwokozi wa ulimwengu, waliendelea kuwa vipofu, wasio tayari kwa mambo ya kuja? Kwa nini ufahamu wao wa msalaba na ufufuo ulikuwa mdogo?

Kwa sababu hawakusikia kwa imani! Mara kadhaa Yesu aliwaadhibu: "Enyi msiofahamu, na wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyosema manabii!" (Luka 24:25).

"Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba?" (Mathayo 8:26). Walikuwa na imani kidogo - mioyo ambayo ilikuwa ya polepole kuamini Neno lake. Nao waliachwa wakiwa tupu, hawakujiandaa, wamechanganyikiwa – wamekuwa vipofu kwa kutokuamini!

Ikiwa Yesu alishangaa kwa kutokuamini kwa wanafunzi wakati alikua hapa duniani, ni nini anapaswa kufikiri kuhusu sisi leo? Ninawi ilitubu baada ya mahubiri moja tu, kwakuamini kila neno ambaloYona alihubiri. Hata hivyo, Amerika imesikia maelfu ya maonyo kama hayo kutoka kwa manabii wengi, lakini watu wengi wanaojazwa na Roho hawawasikiliza. Wanasema, "Sipendi kusikia hilo tena." Nabadaaye wanaliweka nje ya akili!

Je! Unakumbuka kiasi gani cha yale uliyoyasikia? Je, imefanya kazi gani kwa ndani yako ya kiroho? Ikiwa Neno la Mungu halifanyiki na imani - ikiwa hatukumwomba kwa imani ili kutusaidia kupokea na kuitumia - tutaishia kuokota na kuchagua tu kile tunachopenda. Na mara nyingi tunachukua baraka, huruma na faraja na kuondokana na madai, tahadhari na onyo.

Uaminifu hufanya Neno la Mungu lifanye njia yake ndani ya roho yetu. Na imani huiweka ndani ya utu na akili zetu ili iweze kusahau kamwe.