SI KITU CHA BULE KUTOKA KWA ONYO

Carter Conlon

Mtume Petro alitoa neno la onyo kwa watu wa Mungu: "Wapendwa, musione kuwa nia ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba nikitu kigeni kiwapatacho. Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe" (1 Petro 4:12-13).

Aina hii ya ujumbe inaweza kuwa ngumu sana kukumbatia wakati wa amani. Watu wa Mungu wanaweza kukua kwa urahisi na kuwasahau kuwa wanaishi katikati ya jamii ambayo inaweza ghafla, hata kwa ukali, inapingana na Kristo na wafuasi wake.

"Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. Kwa upande wao anatukanwa, lakini kwa upande wenu Yeye ametukuzwa" (1 Petro 4:14).

Kwa maneno mengine, kama dunia inakubali, inamaanisha kwamba wewe ni mmoja wao. Lakini unapofanya uchaguzi wa kuacha ulimwengu ulioanguka, na kukubali mfumo wa thamani wa Neno takatifu la Mungu, maisha yako, mazungumzo yako, moyo wako, na nia zako zote zinabadilika.

Baada ya kusema juu ya jaribio la moto, Petro aliendelea kusema, "Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwizi, au awo kama mtu ajishugulishaye na mambo ya watu wengine" (1 Petro 4:15).

Kabla ya kujishughulisha na msamaha kutoka kwenye onyo hili, kumbuka kwamba lazima tuondoe aina zote za ubaguzi wa rangi na masuala mengine ya kiutamaduni ambayo yanagawanya jamii yetu leo. Lazima tujifunze kusamehe na hatuwezi kuruhusu roho hii ya mauaji na chuki kutupata. Pili, tunapaswa kuwapa badala ya kuwa wachukuwaji. Kisha, tunapaswa kujitenga na uovu. Toka katika uhusiano huo, uondoke klabu hiyo, tupa chini kitabu hicho, uondoke kwenye tovuti hiyo ya mtandao! Ni wakati wa kujitenga na vitu ambavyo vinatupunguza na kutupotosha. Na, mwisho, hatupaswi kuishi kama mtu ajishugulishaye na mambo ya watu wengine - na hiyo ni pamoja na uvumi na kuwa muhimu.

Hebu tuishi kwa namna ambayo upendo wa Kristo unaweza kujulikana kupitia kwetu.

Carter Conlon alijiunga na jopo la wachungaji wa Times Square Church mwaka wa 1994 kwa mwaliko wa mchungaji muanzilishi, David Wilkerson, na alichaguliwa kuwa Mchungaji Mkuu mwaka 2001.