SALA ILIYOONGOZWA NA ROHO YA MUNGU

Jim Cymbala

Paulo aliwaambia waefeso "kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho" (Waefeso 6:18). Nini maneno ya kuvutia na picha ya maneno - kuomba katika Roho. Omba katika Roho, omba katika, kupitia, na kwa Roho Mtakatifu, ambaye ni Mungu mwenyewe!

Kwa kuongeza mufano huu katika Waefeso, kuna mengi: "Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia" (1 Wakorintho 14:15). Juwa kwamba Paulo huomba si kwa mawazo yake tu bali pia kwa roho yake, alichochewa na kuongozwa na Roho wa Mungu.

Ni wapi tena Roho angeweza kufanya kazi hasa kwa roho zetu za kibinadamu? Pia, ili kupigana na wale wanaogawanya Mwili wa Kristo, wale wanaofuata "asili ya tabia za kawaida ni kutukuwa na Roho," Yuda aliwaambia viongozi wake "mkijijenga katika imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika Roho Mtakatifu" (Yuda 20, msisitizo aliongeza).

Maelekezo haya kuhusu sala iliyoongozwa na Roho Mtakatifu inaweza kuonekana kama ushawishi wa kihisia kwa wengine. Wanajisikia ni kwa wale "watu wengine" wanaoimba kila wakati kwa sauti kubwa na kuinua mikono yao kanisani kila sekunde sita. Wanasema, "Hivyo sio jinsi nilivyolelewa kanisani."

Mungu alitupa Biblia ili tuweze kuwa waombaji na kuwa wanyenyekevu, na kutafuta kina chake na uzoefu ambao unaoahadi. Je! Nguvu ya Roho Mtakatifu ili kuhamasisha maobi kwa namna Fulani ili kuenea wakati wa karne zifuatazo kitabu cha Matendo? Je! Roho atatusaidia leo kidogo sana, hasa tunapomhitaji zaidi? Hii haisikiki kama vile Mungu mwenye rehema atakavyofanya.

Tutawezaje kuomba kwa ujasiri kwa imani ikiwa Roho Mtakatifu hajatutusaidia? Tu kama Roho anavyoongoza na kuhamasisha tutainuka kwenye ngazi mpya ya sala iliyopo. Kisha ngome zitaanguka chini, wapendwa watatembelewa na neema ya Mungu, na watu walio karibu nasi watakumbushwa kwamba Kristo ni Mwokozi aliye hai na si mawazo tu ya kitheolojia.

Hakuna kitu kigumu sana kwa Mungu. "Bwana, tufundishe kuomba, na acha iwe sala iko katika Roho Mtakatifu."

Jim Cymbala alianza Hema la Brooklyn (Brooklyn Tabernacle) akiwa na wanachama wasio zidi  ishirini katika jengo la chini katika sehemu ngumu ya mji huo. Mzaliwa wa Brooklyn, yeye ni rafiki wa muda mrefu wa David na Gary Wilkerson.