SABABU YA MUNGU KUONYESHA NGUVU ZAKE

Nicky Cruz

Katika sura ya tatu ya Matendo, baada ya Petro na Yohana kumponya mwombaji kiwete kwenye lango lakuingia ndani ya hekalu, wachache waliokuwa wakiangalia walisimama mbele. Walikuwa wamemjua mtu miaka mingi, na uponyaji haukuweza kuepukika. Watu waliwauliza wanafunzi kuhusu hilo, Petro akawaambia, "Enyi waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utauwa wetu sisi? Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu” (3:12-13).

Wakati Mungu anaamua kuonyesha nguvu zake mbele ya wasioamini, anafanya hilo kwa sababu. Lengo ni kumtukuza Yesu, kuwongoza watu kwa yeye mwenyewe, kutupa maelezo kidogo ya mbinguni itakavyokuwa. Anataka kuonyesha uwezekano wa kushangaza ambao unatarajia kwa wale wanaochagua kumtumikia. Yeye anaonyesha mamlaka yake kamili na yanayozunguka juu ya ulimwengu asili na wakati anachagua kufanya hivyo, sio nafasi yetu ya kuhoji au kutumia hali hiyo. Tunapaswa kukubali na kumpatia ukumbusho na sifa anazostahiki.

Kwa kusikitisha, nimewahi kupata kupinga zaidi nguvu za Mungu zisizo za kawaida kutoka ndani ya mwili wa Kristo, kuliko kutoka nje yake. Waumini wengi huwa na wasiwasi kwa sababu hawajaona Mungu akifanya miujiza kama hiyo katika maisha yao na wana shaka kuwa anafanya hivyo katika maisha ya wengine.

Hii ilinifanya kuwa mwenye wasiwasi sana, lakini sasa ninachagua kusonga mbele, kuendelea kuhudhuria na kuhubiri na kuhamia katika Roho wa Mungu. Ikiwa wengine wanatafuta nguvu na Roho wa Mungu, atawafunulia hilo.

Kusudi ndani ya moyo wako kwamba huwezi kukosa furaha, na nguvu ambayo Kristo anaweza kuleta katika maisha yako. Funguka sana na ukubali hilo!

Nicky Cruz, mwinjilisti wa kimataifa aliyejulikana na mwandishi mkubwa, alimgeukia Yesu Kristo kutokana na maisha ya vurugu na uhalifu baada ya kukutana na David Wilkerson huko New York City mwaka 1958. Hadithi yenye kushangaza ya kuokoka kwake ulisemwa mara ya kwanza katika Musaraba na Kisu kinacho chomoka (Cross and Switchblade) na David Wilkerson na kisha baadaye katika kitabu chake chenye kuliuzwa vizuri, kiitwaco: Kimbiya, Mtuto, Kimbiya (Run, Baby, Run).