PESA YA KODI NDANI YA KINYWA CHA SAMAKI!

David Wilkerson (1931-2011)

Mungu anaweza kurejesha chochote kilichoonekana kilikufa katika maisha yetu kwa neno moja tu. Je! Una matatizo ya kifedha, hauwezi kulipa bili yako? Hivyo vilifika wakati Bwana arikuwa pamoja na wanafunzi wake.

Wakati wa kodi ulipofika, Kristo na wanafunzi wake hawakuwa na pesa kulipa kiasi kinachohitajika. Basi, Bwana alifanyaje kwa kukerebesha hali hiyo? Alimtuma Petro kwenda kuvua samaki. "Nenda baharini, ukatupe ndoano, na uchukue samaki unaokuja kwanza. Na ukifunguwa mdomo wake, utaona chekeli; ichukuwe hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako" (Mathayo17:27).

Ninaweza tu kufikiri ni nini Petro alipaswa kufikiri: "Pesa ya kodi katika kinywa cha samaki? Lazima nione hili. Nimekuwa mvuvi maisha yangu yote na nimeona vitu vingi ndani ya samaki - minyoo, ndoano, mimea ya baharini. Lakini sijawahi kuona sarafu. "Hata hivyo, Petro alipopiga kelele kwenye samaki ya kwanza, alifungua kinywa chake ili kupata sarafu iliyongaa – yenye kutosha kwa kulipa kodi, kama Yesu alivyosema.

Kwa nini Roho Mtakatifu alisukuma waandishi wa injili kurekodi hadithi hii? Na kwa nini Yesu hakuchuwa tu sadaka, au kutuma wanafunzi wake kufanya kazi kwa siku ili kuleta mshahara wa kodi?

Ninaamini Yesu alihamia kwa nguvu hapa kwa sababu alitaka kuthibitisha watoto wake kwamba atafanya jambo lisilowezekana kwetu. Anaweza kurekebisha tatizo lolote! Alitaka tujue yeye ni Mungu yule aliyempa Eliya chakula na nyama iliyotolewa na makungu (1 Wafalme 17:6); aliweka pipa ya mjane wa chakula bila kupungua wakati wa ukame (1 Wafalme 17:14-16); na kulishwa umati wa watu 5,000 na samaki wachache na mikate (Mathayo 14:19-21).

Mungu anajua kwamba wakati fulani katika maisha yetu, muujiza tu atafanya na anataka kutuhakikishia kwamba anaweza kufanya mambo yasiyowezekana kwetu, kwa hali yoyote. Wapendwa, amini Mungu akupeeni katika kila eneo la maisha yako kwa sababu hakuna kitu kisiowezekana kwake.