ONYO DHIDI YA INJILI LOJOLOJO

David Wilkerson (1931-2011)

Nia moja kubwa ya Baba yetu wa mbinguni ni kwamba hakuna " hata injili nyingine" itaweza kutuweka mbali na msalaba wa Yesu Kristo. Wakristo wengi wamepoteza imani yao kwa sababu walipewa neno la kupendeza miaka mingi iliyopita, labda kitu kama hiki: "Utakuwa na huduma kubwa na kushinda maelfu ya roho kwa Bwana," na hakuna hata neno moja liliotimiza hayo. Sasa kondoo hao wamevunjika kabisa, imani yao imejengwa kwenye dundu la majivu.

Ikiwa utapokea neno kutoka kwa Bwana, basi acha liwe lenye kutoka kwa Maandiko. Bora zaidi, basi liwe lenye kutoka kwa wakati wako wa thamani unaotumia ndani ya chumba cha sala pamoja na Yesu. Hebu acha marafiki wako wa karibu wanao mcha Mungu wanajaribu neno hilo pamoja na wewe ili kulithibitisha; Vinginevyo, ikiwa unaruhusu chochote kupata njia ya injili ya kweli, utaishia kwa kukata tamaa.

Paulo alikuwa na wasiwasi juu ya uvamizi wa hatari dhidi ya kanisa la Kristo wakati aliwaambia Waefeso: "Na miongoni mwenu watu watainuka, wakisema maneno mapotovu, ili wajipatie wanafunzi wanaowafuata" (Matendo 20:30). Neno la Kiyunani kwa "kupotoka" hapa linamaanisha kuendelea kushikilia kwa kueneza kosa.

Paulo alikuwa akionya, "Wengine wenu katika mamlaka watainuka na kuleta injili iliyopotoka, kwa kuanzisha rushwa ndani ya injili safi." Je! Hii iliwezekanaje kutokea kati viongozi wa kanisa hili? Angalia, Paulo hakuwa akizungumzia mbwa mwitu au wezi wa wajane. Hapana, alikuwa akimaanisha wahudumu ambao wanajitahidi na kurudi nyuma kutoka kwa kuhubiri shauri lote la Mungu - wale wanaowasilisha injili ya lojolojo, nusu ya injili, ni sehemu tu ya Neno la Mungu.

Ni wajibu wa kila muumini kuwa na uhakika wa kukaa chini ya mafundisho ya mchungaji mwema, anayehubiri ukweli wote, Neno la Mungu lisilo na dosali. Yesu anasema, "Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema hutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo" (Yohana 10:11). Hii ina maana kwamba mtumishi wa Mungu ataweka kiburi chake chote chini na hofu ya mwanadamu ili kulisha kundi lake Neno la Mungu safi. Kuwa na uhakika usitegeme kitu kidogo.