NJIA YA MUNGU

David Wilkerson (1931-2011)

Hali ya shida na hali ya msuko suko inaweza kuleta kuchanganyikiwa. Katika nyakati hizo, kutovumilia kwetu huanza kufikiri: "Mungu lazima asimaanishe kile aliniambia mimi au labda shida ni kukosa uwezo wa kusikia sauti yake Labda nilisikia vibaya wakati aliniita mara ya kwanza. aliniambia na kile ninachokiona kuendeleza usiongeze.”

Wakati Sauli alipokuwa akiendelea mbele ya mwongozo wa Mungu, alitendaa kwa usahihi na kuwaza, si kwa kuamini. Sikilizeni kamba la udhuru alimpa nabii Samweli kwa kuendeleza mwongozo wa Mungu: "Nikwasababu niliona ya kuwa watu wanataanyika mbali name,na wewe hukuja siku zile zilizonenwa; nawo waflisti wamekusanyika pamoja huko Mikmash,basi nikasema,Wafilisti watanishukia sasa mpaka Gilgali, kabla sijaomba fadhili za BWANA; kwa hiyo nalijishurutisha,nikatoa sadaka ya kuteketezwa" (1 Samweli 13:11-12). Sauli alichukua mambo kwa mikono yake mwenyewe, akifanya kile alichokifikiri kuwa chaguo lake peke. Na ikaisha kwa huzuni.

Suala hili la kusubiri ni muhimu sana kwamba tunapata kumbukumbu juu yake katika Neno la Mungu. Isaya anaandika, "Katika siku hiyo watasema:" Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, ndiye tuliyemngojea atusaidie, "Huyu ndiye BWANA, tuliyemngojea, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake” (Isaya 25:9).

"Maana tangu zamani za kale watu wakasikia,wala kufahamu kwa masikio,wala jicho halikuona Mungu, ila wewe atenaye mambo kwa ajili yake amngojaye" (Isaya 64:4).

Wapendwa, njia ya Mungu sio njia ya ulimwengu. Na njia pekee ya kupata uzoefu wa kimungu ni kumngoja kwa subira ndani ya imani. Tabia hii ya uzoefu wa kimungu huja kwa wale walio katika ushirika na Bwana: "Mukijua ya kuwa dhiki, kazi yake nikuleta saburi; nakazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini" (Warumi 5:3-4).