NJE YA NYAKATI ZA GIZA

David Wilkerson (1931-2011)

Nabii Isaya anatuonya kwamba katika siku za mwisho Mungu ataka "kugeuza ulimwengu upunguke." Anasema, "Tazama, Bwana huifanya dunia kuwa tupu, na kuiharibu, na kuipindua" (Isaya 24:1, KJV). Kwa mujibu wa unabii huu, hukumu ya ghafla inakuja juu ya dunia na kila kitu ndani yake kitabadirika katika muda mfupi sana. Ubinadamu utashuhudia uharibifu wa haraka juu ya jiji na taifa, na ulimwengu hautakuwa sawa.

Ikiwa umeunganishwa na vitu vya kimwili - ikiwa unapenda dunia hii na vitu vyake - hutaki kusikia kile Isaya ametabiri. Kwa hakika, hata kwa wenye haki zaidi ya watu wa Mungu, kile Isaya anachosema inaweza kuwa kisichowezekana; wengi bila shaka watauliza, "Je! ulimwengu mzima unaweza kuanguka katika saa moja?" Maandiko yanasema wazi: Dunia itabadilika; kanisa litabadilikq; kila kitu kimojakimoja duniani kitabadilika.

Katika unabii wa Isaya, mji kuwa chini ya hukumu nikutupwa katika machafuko: "Mji wa ;qchqfuko umebobomolewa; kila nyumba imefungwa, ili mtu asiingie" (Isaya 24:10). Ndani ya mji umebaki ukiwa (tazama 24:12).

Wakati Mnala wa Mapacha (Twin Towers) katika mji wa New York wakati ulishambiliwa, moto na moshi vya ajabu vilionekana hewani mbali sana. Isaya haonyeshi jiji ambalo hukumu ya uharibifu itashukia, lakini jiji lolote kubwa duniani litakabiliwa.

Unaweza kuuliza, "Nini kuhusu watu wa Mungu katikati ya haya yote?" Katika masaa ya giza, sauti zenye kuimbwa duniani kote zitaimbwa kwa sifa kwa ajili ya utukufu wa Mungu: "Hawa watainuwa sauti zao, wataimba kwa sauti kubwa; kwa sababu ya utukufu wa Bwana watapiga kelele kutoka baharini" (24:14).

Hii ndiyo matumaini ya imani yetu takatifu zaidi: Bwana wetu hufanya wimbo utoke katika wakati wa giza. Anza sasa kujenga imani yako takatifu ndani yake na kujifunza kusifu utukufu wake kimya kimya moyoni mwako. Unapoimba wimbo wako, itaimarisha na kuwatia moyo ndugu zako na dada zako, na utawushuhudia ulimwengu: "Bwana wetu anatawala juu ya gharika" (Zaburi 29:10). Haleluya!