NDANI YA MACHO YA BABA

David Wilkerson (1931-2011)

Ninaposema imani kamili katika Kristo, simanishi tu katika nguvu zake za kuokoa lakini pia katika uwezo wake wa kuweka. Tunatakiwa kuamini Roho wake ili atuhifadhi na kutufananisha na mfano wa Kristo.

Wakati mmoja ulikuwa mbali, ukatwa na Mungu kwa kazi mbaya. Ulifanya kazi gani nzuri ya kufanya mambo sawa na yeye? Hakuna! Hakuna aliyewahi kufanya au kujitunza mwenyewe. Tunaletwa katika utakatifu wa Kristo kwa imani peke yake, kama tunavyoamini katika kile ambacho Neno la Mungu linasema: "Ikiwa mmekuwa ndani ya Kristo, nanyinyi ni watakatifu kama yeye yu mtakatifu."

"Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete nyinyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama – mkidumu tu katika ile imani" (Wakolosai 1:21-23).

Weka uyu musitali, "Ikiwa utaendelea katika imani." Yesu anasema, "Endeleeni kunitegemea, na kuishi kwa imani, nitakutambulisha wewe kama musafi, asiye na hatia, kama mtakatifu mbele ya Baba."

Wapendwa, hii ndiyo kazi yote ya utakaso ya Roho Mtakatifu. Kama Roho inakuwezesha wewe kuacha matendo ya mwili, atakuongoza kwa ushawishi wake.

Hakuna viwango vya utakatifu, kuna viwango vya ukomavu ndani ya Kristo. Unaweza kuwa Mkristo mpya na bado kuwa mtakatifu kabisa ndani ya Yesu. Kwa hivyo usilinganishe! Ni upumbavu kupima mwenyewe dhidi ya mtu unayemwona kama "mtakatifu." Sisi sote tunapimwa kwa kiwango kimoja, utakatifu wa Kristo. Na ikiwa tuko ndani yake, utakatifu wake ni wetu kwa kipimo sawa.

Kamwe usione tena kiongozi mwingine wa Kikristo na kusema, "La, ningelipenda kuwa mtakatifu kama alivyo!" Huwezi kuwa na nidhamu ya mtu huyo au maisha yake ya maombi na unaweza kukabiliana mara nyingi zaidi kuliko yeye. Lakini yeye hakubaliwi sana na Baba kuliko wewe.